Kigonigoni ni kata ya Wilaya ya Mwanga iliyopo karibu na mpaka wa Kenya katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2022, kata ilikuwa na wakazi wapatao 3,325 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 2,610 [2] walioishi humo. Aidha Kigonigoni ndiyo makao makuu ya tarafa ya Jipendea.

Ndiyo kata yenye shule ya Advanced Level kwa upande wa tambarare ya mashariki.

Vijiji hariri

Kata ina vijiji vinne, ambavyo ni: Kigonigoni, Butu, Kwakihindi na Ruru.

Shughuli hariri

Shughuli kubwa za wakazi wa kata hii ni kilimo, ufugaji na uvuvi ndani ya Ziwa Jipe.

Kijiji ambacho wananchi wake wanajishughulisha na uvuvi kwa asilimia 90 ni kijiji cha Ruru.

Makabila hariri

Kabila kubwa linalopatikana katika kata hii ni Wapare. Yapo makabila mengine kama Wakamba na Wachaga ingawa makabila hayo ni kama yamemezwa na Wapare.

Dini hariri

Wakazi wengi ni wafuasi wa dini ya Uislamu na ya Ukristo.

Utamaduni hariri

Watu wake hupendelea mlo wa ugali kwa samaki mara nyingi pamoja na makande, kutembeleana wakati wa sikukuu za kidini, Kushirikiana shughuli za msiba au ugonjwa.

Michezo kwao ni mpira wa miguu hasa kwa walio vijana zaidi.

Mipaka hariri

Upande wa mashariki kata hii inapakana na nchi ya Kenya, mwambao wa ziwa Jipe. Upande wa magharibi inapakana na safu ya milima ya Upare (Usangi). Upande wa kaskazini inapakana na kijiji cha Mkisha. Upande wa kusini inapakana na vijiji vya Kwakoa na Toloha.

Vivutio hariri

1. Ndiva yefuka katika Mto Mala. 2. Ziwa Jipe mpakani mwa Kenya na Tanzania.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Kilimanjaro - Mwanga DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-27.
  Kata za Wilaya ya Mwanga - Mkoa wa Kilimanjaro - Tanzania  

Chomvu | Jipe | Kifula | Kighare | Kigonigoni | Kileo | Kilomeni | Kirongwe | Kirya | Kivisini | Kwakoa | Lang'ata | Lembeni | Mgagao | Msangeni | Mwanga | Mwaniko | Ngujini | Shighatini | Toloha

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kilimanjaro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kigonigoni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Isipokuwa usitaje majina ya viongozi waliopo sasa maana wanabadilika haraka mno.