Konrado wa Piacenza

(Elekezwa kutoka Konradi Confalonieri)

Konrad wa Piacenza (jina lake kwa Kiitalia lilikuwa Corrado Confalonieri), ambaye alizaliwa Piacenza, Emilia-Romagna, Italia, 1290 hivi, akafariki Noto, Siracusa, Sicilia, Italia visiwani tarehe 19 Februari 1351, alikuwa mkaapweke wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu mwaka 1625.

Konrad Confalonieri wa Piacenza.

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake.

Maisha

hariri

Konrad alizaliwa katika moja ya familia maarufu zaidi ya mji wa Piacenza, akamuoa Efrosina akiwa kijana sana, akiendelea na maisha ya tabaka lake pamoja na kuzingatia dini ya Ukristo.

Kisha mwenyewe kusababisha bila makusudi uharibifu mkubwa kwa moto, mkulima aliyepita huko alikamatwa, akateswa na kisha kulazimishwa kukiri kosa asilolifanya akahukumiwa kufa.

Alipomuona anapelekwa kuuawa, Konrad alikiri kosa lake, na kama fidia alilazimika kuuza maali yake yote.

Yeye na mke wake walioona mkono wa Mungu katika tukio hilo, wakakubaliana kutengana ili kutawa, mmoja mahali pa upweke pa Wafransisko wa Utawa wa Tatu, mwingine katika monasteri ya Waklara.

Mapema alijulikana kwa utakatifu, hivi kwamba umati wa watu waliomtembelea ulimzuia asifaidike zaidi na maisha ya upwekeni aliyojitafutia.

Hapo alifika Roma, na kutoka huko akahamia Noto, Sicilia, alipoishi upwkeni kwa miaka 36 kwa toba kali, akitenda miujiza mingi hadi kifo kilipomkuta akiwa anasali mbele ya sanamu ya Yesu msalabani.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: