Mitragyna speciosa

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Asterids (Mimea kama alizeti)
Oda: Gentianales (Mimea kama mwadiga)
Familia: Rubiaceae (Mimea iliyo mnasaba na mbuni)
Jenasi: Mitragyna
Korth.
Spishi: M. speciosa
(Korth.) Havil.

Kratom (jina la Kilatini: Mitragyna speciosa) ni mti wa kijani wa kitropiki katika familia ya kahawa (Rubiaceae) wenye asili ya kusini mashariki mwa Asia. Mti huu unapatikana kwa wingi nchi za Thailand, Indonesia, Malaysia, Myanmar, na Papua New Guinea ambako umetumika kama dawa ya asili tangu karne ya 19.

Hadi mwaka wa 2018, hakuna majaribio ya kisayansi yaliyofanywa ili kuelewa madhara ya kratom kwa afya.[1] Baadhi ya watu hutumia mti huu kama dawa ya kupunguza maumivu ya muda mrefu, kwa kutibu madhara ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kama heroini, opioidi au kwa ajili ya burudani.

Madhara madogo ya kawaida yanayotokana na mti huu ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, na kuvimbiwa. Madhara makubwa ni pamoja na shinikizo la damu, kuwa mteja wa kudumu wa dawa hii, shida ya kulala, sumu ya ini. Mti huu huweza pia kusababisha kifo. Nchini Marekani, kulikuwa na vifo kumi na tano kutokana na matumizi ya kratom kati ya mwaka 2014 na 2016. Matumizi yake ni kinyume cha sheria kwenye nchi mbalimbali za Ulaya kama vile Uingereza na Ufaransa. Nchini Marekani majimbo yake yana sheria zinazotofautiana kidogo kuhusu matumizi yake.

Kwenye jamii ambako mti huu unapatikana, Kratom imekuwa ikitumika kama dawa ya asili au mitishamba. Majani yake hutafunwa kupunguza maumivu ya mifupa na kuongeza nguvu, hamu ya chakula na matamanio ya kujamiiana kama vile miraa na kokaini. Majani yake hutumika kutibu majeraha. Hutumika pia kutibu kikohozi, kuharisha na matatizo ya tumbo. Majani yake hutumiwa pia na wafanyakazi wa kazi ngumu ili kuondoa uchovu. Tofauti za matumizi yake hutegemea pia aina za mti wenyewe maana kuna aina mbalimbali zinazotofautiana kati ya nchi na nchi. Huko Thailand Kratom ilitumika kama kitafunio cha kukaribisha wageni na pia ilitumika kwenye ibada za miungu ya jadi.[2]

Marejeo

hariri
  1. Warner ML, Kaufman NC, Grundmann O (2016). "The pharmacology and toxicology of kratom: from traditional herb to drug of abuse". Int. J. Legal Med. (Review). 130 (1): 127–38. doi:10.1007/s00414-015-1279-y. PMID 26511390.
  2. Singh, Darshan; Narayanan, Suresh; Vicknasingam, Balasingam (Septemba 2016). "Traditional and non-traditional uses of Mitragynine (Kratom): A survey of the literature". Brain Research Bulletin. 126 (Pt 1): 41–46. doi:10.1016/j.brainresbull.2016.05.004. PMID 27178014.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kratom kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.