Open main menu

Msingi katika imaniEdit

Adhimisho hilo la liturujia ni la zamani, lakini limepata nguvu mpya kutokana na dogma iliyotangazwa na Papa Pius XII kwa hati Munificentissimus Deus ya tarehe 1 Novemba 1950 baada ya kusikiliza maoni ya maaskofu wote duniani.

Fundisho hilo la imani Katoliki ni kwamba Bikira Maria, mama wa Yesu, alipomaliza maisha yake duniani alichukuliwa mwili na roho mbinguni, ashiriki mapema utukufu wa Mwanae mfufuka, Yesu Kristo kama alivyoshirikiana naye toka mwanzo hadi mwisho wa maisha yake.

Fundisho hilo linalingana na lile la Waorthodoksi, ingawa hao hawajalitangaza kuwa dogma. Tarehe hiyohiyo wao wanaadhimisha ya Kulala kwa Bikira Maria.

Hata baadhi ya Waanglikana na Walutheri wana adhimisho la Bikira Maria siku hiyo.

Umoja wa msimamo huo upande wa mashariki na wa magharibi wa Kanisa unatokana na mapokeo ya karne za kwanza za Ukristo, yanayoshuhudiwa na mababu wa Kanisa kama vile Efrem wa Syria, Timoteo wa Yerusalemu, Epifanio wa Salamina na Yohane wa Damasko.

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria kupalizwa mbinguni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.