Katoliki
Katoliki kwa Kiswahili limetokana na neno la Kigiriki καθολικός (katholikos), maana yake "kadiri ya utimilifu", "zima". [1]
Katika eklesiolojia ya Ukristo, jina hilo lina historia ndefu na matumizi tofauti kadhaa.
Kwa wengine, neno "Kanisa Katoliki" linahusu Kanisa ambalo lina ushirika kamili na Askofu wa Roma (maarufu kama Papa) na linaloundwa na umoja wa madhehebu ya Kilatini na mengine 23 ya Makanisa Katoliki ya Mashariki: ndiyo matumizi ya kawaida katika nchi nyingi. Waumini wake wengi hawajibaini kama "Waroma", lakini kama "Wakatoliki" tu.
Wakatoliki na vilevile Waorthodoksi wanaamini kwamba Kanisa lao ni la kwanza na ndilo Kanisa lenyewe.
Waanglikana, Walutheri na baadhi ya Wamethodisti huamini kuwa makanisa yao ni ya Kikatoliki kwa maana ya kwamba yako katika mwendelezo na asili ya Kanisa la kimataifa lililoanzishwa na Mitume wa Yesu.
Waprotestanti wakati mwingine hutumia neno "Kanisa Katoliki" kwa kutaja waumini wote wa Yesu Kristo duniani, bila kujali "madhehebu" kuyaunganisha.
Katika mwelekeo wa Kikatoliki (ikiwa ni pamoja na Ushirika wa Kianglikana), maaskofu wanachukuliwa kuwa ndio wenye daraja ya juu ndani ya dini ya Kikristo, kama wachungaji wa umoja katika ushirika na Kanisa lote na miongoni mwao. [2]
Ukatoliki hufikiriwa kuwa moja ya sifa za Kanisa, nyingine zikiwa umoja, utakatifu na utume. [3] kulingana na Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli ya mwaka 381: "Nasadiki Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume."
Historia ya matumizi ya neno "Katoliki"
haririKatika Karne ya 2
haririBarua zilizoandikwa na Ignas wa Antiokia kwa Wakristo wenzake wa sehemu mbalimbali [4]mwaka 106 hivi ni ushahidi wa awali wa matumizi ya neno Kanisa Katoliki (Barua kwa Wasmirna, 8). Kwa kusema Kanisa Katoliki Ignas alitaja kanisa zima katika ushirika na Kanisa la Roma "linalosimamia upendo".
Ignas aliandika kwamba baadhi ya wazushi wa wakati wake, ambao hawakuamini kwamba Yesu aliteswa na kufa, wakisema badala yake kwamba "yeye alionekana tu kuteseka" (Barua kwa Wasmirna, 2), hawakuwa Wakristo wa kweli. [5]
Neno hili pia hutumika katika "Kifodini cha Polikarpo" mwaka 155 na katika "Hati ya Muratori" mwaka 177.
Sirili wa Yerusalemu
haririSirili wa Yerusalemu (kama 315-386) aliwataka wale aliokuwa akiwafunza katika imani ya Kikristo: "Kama wewe saa yoyote unakaa katika miji, usitafute tu mahali ambapo 'nyumba ya Bwana' ipo (kwani madhehebu mengine pia huvunja wito wao wakiita maabadi yao 'nyumba ya Bwana'), wala si kanisa, lakini ulizia Kanisa Katoliki. Kwa kuwa hilo jina ni la pekee kwa Kanisa takatifu, mama yetu sote, ambaye ni bibi arusi wa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu" (Katekesi, XVIII, 26). [6]
Theodosius Mkuu
haririNeno Ukristo wa Kikatoliki liliingia sheria za Dola la Roma wakati Theodosius Mkuu (Kaisari miaka 379-395) alipotuza jina hilo kwa ahali ya "kuwa dini ambayo ilikuwa mikononi mwa Warumi na Mtume Petro, kama ilivyohifadhiwa na waamini kimapokeo na ambayo ni sasa nadhiri kwa Papa Damas na kwa Askofu Petro wa Alexandria... Kuhusu wengine, ambao katika hukumu yetu ni wajinga, sisi tunaamuru wapewe jina la wazushi, wala hawatapata kuita nyumba zao kwa jina la makanisa."
Sheria hii ya tarehe 27 Februari 380, iliyoorodheshwa katika Kitabu cha 16 cha Codex Theodosiania, [7] iliimarisha Ukristo wa Kikatoliki kama dini rasmi ya Dola la Roma.
Agostino wa Hippo
haririMatumizi ya neno Katoliki kwa lengo la kutofautisha Kanisa la "kweli" kutoka makundi ya uzushi hupatikana pia katika Agostino wa Hippo (354-430) aliyeandika:
- "Katika Kanisa Katoliki, kuna mambo mengine mengi ambayo huniweka karibu nalo. Ridhaa ya watu na mataifa hunitunza katika Kanisa; pia mamlaka yake, ambayo ilianzishwa kwa miujiza, na kulishwa na tumaini, na kuongezwa kwa upendo, ulioimarishwa na umri. Mlolongo wa maaskofu huniweka mimi, mwanzo kutoka kiti cha Mtume Petro, ambaye Bwana, baada ya kufufuka kwake, akampa mamlaka kulisha kondoo zake (Yoh 21:15-19), chini ya sasa Uaskofu (katika Roma: hapa Agostino anazungumza juu ya urithi wa Papa).
- "Na hivyo, mwisho, je sana jina la "Katoliki", ambalo, si bila sababu, huku kukiwa na uzushi mwingi, Kanisa linabakia hivyohivyo kwamba, ingawa wazushi wote wanataka kuitwa Wakatoliki, lakini wakati ambapo mgeni anauliza wapi Kanisa Katoliki hukutana, hakuna mzushi anayethubutu kumpeleka nyumbani kwake.
- "Hivyo basi idadi na umuhimu ni mahusiano ya thamani ya mali kwa jina la Kikristo ambayo humweka muumini katika Kanisa Katoliki, kama haki inavyopasa ... Pamoja nanyi, ambapo hakuna mambo haya kunivutia au kuniweka ... Hakuna mtu atakayenihamisha kutoka imani ambayo inahusu akili yangu pamoja na mahusiano ya wengi na hivyo nguvu ya dini ya kikristo ... Kwa upande wangu, singeweza kuamini Injili kama nisingeoongozwa na mamlaka ya Kanisa Katoliki."
- Dhidi ya Waraka wa Wamani inayoitwa Msingi, sura ya 4: kuhusu Imani Katoliki. [8]
Vincent wa Lerins
haririMtakatifu mwingine aliyeishi wakati wa Agostino, Vincent wa Lerins, aliandika mwaka 434 (akitumia jina Peregrinus) kitabu kinachojulikana kama Commonitoria ("Kumbusho").
Humo alisisitiza kwamba, kama mwili wa binadamu, mafundisho ya Kanisa huendeleza ukweli huku yakitunza utambulisho wake (mstari 54-59, sura XXIII): "Katika Kanisa Katoliki lenyewe, tuwe waangalifu iwezekanavyo, kwamba sisi hushikilia imani ambayo imekuwa ikiaminiwa kila mahali, daima, na wote. Kwa kuwa ni kweli na katika 'Katoliki', ambayo kama jina lenyewe na sababu ya kutangaza kitu, unaoeleweka na kila mtu. Utawala huu tutakuwa tumeuzingatia kama tutafuata umoja katika ulimwengu, muda, ridhaa. Tutafuata umoja kama tunakiri kwamba imani moja kuwa kweli, ambayo Kanisa zima duniani kote tunakiri; muda, kama sisi tusikose busara tukaondoka kutoka tafsiri ya mababu wetu; kukubali, katika namna, kama sisi wenyewe katika zamani kuambatana na ridhaa, ufafanuzi na bidii ya wote, au wa madaktari wa mapadri wote" (sehemu 6, mwisho wa sura II).
Wakatoliki wa Magharibi na wa Mashariki
haririMadhehebu ya Kanisa Katoliki (Kanisa la Kilatini na Makanisa Katoliki ya Mashariki ishirini na tatu) huwa na jukumu la kuhifadhi mapokeo Katoliki ya Mababu wa Kanisa la mwanzo.
Makanisa Katoliki ya Mashariki ni yale makanisa ambayo yako katika ushirika kamili na Askofu wa Roma (Papa), huku wakiwa wanajitegemea (kwa lugha ya Kilatini ni Ecclesiae sui iuris) kwa kulinda taratibu za liturujia, za teolojia na mapokeo ya makanisa mbalimbali ya Ukristo wa Mashariki ambayo wanahusishwa nayo.
Madhehebu hayo ni kama vile yale ya Wagiriki, Waukraina, Warutheni, Wamelkiti, Wakopti, Waethiopia, Wamaroni, Wasiro-Malankara, Waarmenia, Wakaldayo na Wasiro-Malabari.
Chini ya Papa Yohane Paulo II Kanisa Katoliki lilitoa kitabu cha mafundisho ya imani na maadili chenye kichwa Katekisimu ya Kanisa Katoliki ambacho kinasema: "Kuamini kwamba Kanisa ni 'takatifu' na 'Katoliki,' nalo ni 'moja' na 'la Mitume '(kama Kanuni ya Imani ya Nisea inavyodokeza), hakuwezi kutengwa na imani katika Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. [9]
Neno Kanisa Katoliki linahusu Kanisa lote linaloongozwa na Askofu wa Roma, sasa Papa Fransisko, na ambalo lina zaidi ya waumini bilioni 1.2, wakiwa nusu ya Wakristo wote duniani, wanaokadiriwa kuwa bilioni 2.4.
Ingawa kawaida Kanisa Katoliki linajitofautisha na makanisa mengine kwa kujiita "Kanisa Katoliki" tu, pengine linakubali kutumia ufafanuzi "Kanisa Katoliki la Roma", hasa katika hati zilizoandaliwa pamoja na makanisa mengine, lakini pia katika Nyaraka kadhaa za Kipapa [10] [11]
Mfano mwingine ni ufafanuzi kama Kanisa Takatifu, Katoliki, la Kirumi la Kitume [12] katika Katiba Katoliki ya Mtaguso wa kwanza wa Vatikano ya tarehe 24 Aprili 1870. Kurasa hizi zote zinahusu Kanisa Katoliki na kwa majina mengine.
Makanisa Katoliki ya Mashariki, ingawa yana umoja na Roma katika imani, taratibu na sheria zake, yanatofautiana na madhehebu ya Kilatini na Makanisa Katoliki mengine ya Mashariki.
Matumizi mbalimbali
haririBaadhi ya Makanisa ya Kikristo, hasa Makanisa ya Waorthodoksi, wanajiona kuwa kweli Kanisa Katoliki ambalo, katika mtazamo wao, Wakristo wengine wote, wakiwa pamoja na wale walio katika ushirika na Papa, walijitenga mbali.[13]
Mbali ya Kanisa la Kiorthodoksi[14], Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki na Kanisa la Waashuru hujiona pia kama "Kanisa Katoliki moja Takatifu la kitume" la Kanuni ya imani ya Nisea.
Waanglikana na Wakatoliki wa Kale hujiona katika ushirika katika Kanisa moja na Walutheri wenyewe kama ni "harakati ya mageuzi makubwa ndani ya Kanisa Katoliki".
Wakati Wakatoliki wa Kirumi humwona Askofu wa Roma kama "Halifa wa Petro" anayepaswa kutumikia kama mchungaji wa Kanisa zima, Waanglikana na Wakatoliki wa Kale hukubali kuwa Askofu wa Roma ni Primus inter Pares kati ya Waprimati wote, lakini wao hukumbatia Usinodi ili kujikinga dhidi ya Ultramontanism.
Juhudi za hivi karibuni za Kanisa Katoliki hulenga kuponya mgawanyiko kati ya makanisa ya Magharibi ("Katoliki") na Mashariki ("Orthodoksi"). Papa Yohane Paulo II mara nyingi alizungumza hamu yake kubwa kwamba Kanisa Katoliki "lirudi kupumua kwa mapafu yote mawili", [15] [16] na hivyo kusisitiza kwamba Kanisa Katoliki linataka kurejesha ushirika kamili na Makanisa ya Mashariki yaliyotengana nalo. [17]
Ni kwamba, baada ya utengano wa Mashariki-Magharibi mwaka 1054, muungano mfupi ulikubaliwa kati ya Papa na baadhi ya Maaskofu wa Kiorthodoksi. Hata hivyo, mkataba huu ulikataliwa na mmoja wa Maaskofu wa Mashariki, yaani Marko wa Efeso, na watu wa kawaida kwa jumla walikataa mkataba huo.
Papa Benedikto XVI amesema nia yake ya kurejesha umoja kamili na Waorthodoksi. Kanisa Katoliki linazingatia kwamba karibu tofauti zote zimesuluhishwa (katika kifungu cha Filioque, suala la purgatorio, n.k.), na alitangaza kwamba tofauti katika desturi za jadi, taratibu na nidhamu si vikwazo kwa umoja. [18]
Wakristo wengine wa Magharibi
haririMakanisa mengi ya Matengenezo ya Kiprotestanti hutumia neno la kikatoliki kurejea kwa imani kwamba Wakristo wote ni sehemu ya Kanisa moja bila kujali madhehebu; kwa mfano, mlango wa 25 wa Ukiri wa Imani wa Westminster unataja kanisa katoliki au la mahali popote (universal)[19].
Viongozi wa matengenezo walitumia neno la kikatoliki kwa maana asili ya "la mahali popote na wakati wowote" siyo kwa dhehebu au mamlaka fulani ndani ya Ukristo. Walijiona wanaendeleza mapokeo ya kanisa lilipokiri "Kanisa moja, takatifu, katoliki, la Mitume" katika Kanuni ya Imani ya Nisea. Hii inalingana pia na kanisa takatifu Katoliki katika kanuni ya Imani ya Mitume.
Neno hili pia linaweza kumaanisha yale makanisa ya Kiprotestanti ambayo hudumisha Uaskofu wao tangu wakati wa mitume na kujiona sehemu ya Kanisa la kikatoliki. Miongoni mwa wale ambao hujiona kama sehemu ya Kanisa la kikatoliki, lakini si Katoliki, ni Waanglikana na baadhi ya Makanisa ya kikatoliki yaliyogawanyika katika karne ya 19 na 20, kama vile Kanisa Katoliki la Kale na Kanisa Katoliki huru, hujifikiria kuwa Wakatoliki, tena Wakatoliki wa kweli wa Kirumi.
Neno linaweza kurejea umoja (idadi) wa Kanisa kwamba, kulingana na Math 16:18-19 Yesu alimwambia Mtume Petro: "Na mimi nakwambia, wewe ni כיפא (Kepha) (kwa Kiaramu "mwamba"), na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, na nguvu za kifo hazitalishinda. Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na kila utakachofunga duniani kitafungwa mbinguni, na lolote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."
Baadhi hutumia wa kikatoliki ili kutofautisha msimamo wao na ule wa Wakalvini au namna ya Uprotestanti uliorekebishwa. Hii ni pamoja na Waanglikana, mara nyingi pia hujulikana Waanglikana wa Kikatoliki, na Walutheri kadhaa ambao husisitiza kwamba wao ni Waprotestanti na wa kikatoliki pamoja.
Wamethodisti na Wakalvini hudai madhehebu yao hutokana na Mitume na kanisa la kwanza, lakini hawawezi kudai kushuka kutoka kanisa la kale katika miundo kama vile Uaskofu. Hata hivyo, makanisa hayo hukiri kwamba wao ni sehemu ya kanisa la kikatoliki (zima). Waanglikana na Wamethodisti, hasa wa Marekani, wameitwa mara nyingi kwa utani Wakatoliki Wepesi. [20] [21]
Hata hivyo, mara nyingi makanisa ya Kiprotestanti yaliachana na neno la Kigiriki "katoliki" na kutumia tafsiri katika matoleo yao ya Kanuni za Imani ya Mitume au ya Nikea. Pamoja na nia ya kutumia lugha inayoeleweka kirahisi zaidi yaliona pia haja ya kuepukana na neno linalotazamwa na wengi kama la kidhehebu. Hivyo kwa Kiswahili Walutheri hutumia lugha "Kanisa takatifu la Kikristo lililo moja tu" wakati Wamoravian hutumia "Kanisa takatifu lililopo popote". Waanglikana hutumia umbo "kanisa katholiko", si "katoliki".
Kuepuka matumizi
haririBaadhi ya makanisa ya Kiprotestanti huepuka kutumia neno hilo kabisa, kwa mfano Walutheri wengi hutumia neno la Kikristo badala ya la kikatoliki. [22] [23] [24] Makanisa ya Orthodox huelewa hisia kuhusu madai kipapa Katoliki, lakini kutokubaliana na baadhi ya Waprotestanti juu ya asili ya kanisa kama mwili mmoja.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ (taz. Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon)
- ↑ FL Msalaba, Oxford Dictionary la Kanisa la kikristo, 1977:175.
- ↑ Christliche Religion, Oskar Simmel Rudolf Stählin, 1960, 150
- ↑ J. H. Srawley (1900). "Ignatius Epistle to the Smyrnaeans". Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
- ↑ "Kama makafiri wanakariri kwamba Yeye alionekana tu kuteseka, basi wao wenyewe wanaonekana tu kuwa Wakristo". Ignas alisema wazushi hao hawakuamini ukweli wa mwili wa Kristo, ambao ulimfanya ateseke halafu akafufuka: "Wao hawakiri Ekaristi kuwa mwili wa Mwokozi wetu Yesu Kristo, ambaye aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, na ambayo Baba, kwa wema wake, alimfufua tena" (Barua kwa Wasmirna, 7). Hivyo akawaita "wanyama katika sura ya watu, ambao lazima si kutowapokea tu, lakini, kama inawezekana, hata kutokutana nao" (Barua kwa Wasmirna, 4).
- ↑ "Catechetical Lecture 18 (Ezekiel xxxvii)". Trinity Consulting. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
- ↑ Paul Halsall (1997). "Banning of Other Religions Theodosian Code XVI.i.2". Internet Medieval Sourcebook. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-27. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
{{cite web}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ Augustine of Hippo (397). "Against the Epistle of Manichaeus called Fundamental". Christian Classics Ethereal Library. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
- ↑ Katekismi ya Kanisa Katoliki, 750
- ↑ Divini illius Magistri
- ↑ Humani generis.
- ↑ Pope Pius IX (1870-04-24). "First Vatican Council – Session 3: Dogmatic constitution on the Catholic faith". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-02-07. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
{{cite web}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Basic Principles Of The Attitude of The Russian Orthodox Church toward the Other Christian Confessions, adopted by the Jubilee Bishops’ Council of the Russian Orthodox Church, 14 Agosti 2000
- ↑ Katikismi ndefu ya Orthodox, Katoliki, Kanisa la Mashariki.
- ↑ Encyciclical Ut unum Sint, 54
- ↑ Apostolic Succession Sacri Canones
- ↑ obituary ya Papa Yohane Paulo II
- ↑ Second Vatican Council Decree on Ecumenism 16
- ↑ https://en.wikisource.org/wiki/The_Confession_of_Faith_of_the_Assembly_of_Divines_at_Westminster#Chapter_25
- ↑ "Diet Catholic". Everything2.com. 2000-03-30. Iliwekwa mnamo 2009-05-28.
- ↑ "Methodist vs Catholic - Catholic Answers Forums". Forums.catholic.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 2009-05-28.
- ↑ "Nicene Creed". The Lutheran Church, Missouri Synod. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-02-02. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
- ↑ "Nicene Creed". Wisconsin Evangelical Lutheran Synod. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-02. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
- ↑ "Nicene Creed". International Lutheran Fellowship. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-09-28. Iliwekwa mnamo 2007-06-24.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Katoliki kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |