Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

  • usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
  • usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
  • usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
  • usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
  • do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

--Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:38, 6 Machi 2021 (UTC)Reply

Ndugu asante kwa mchango wako Celestine ukwu. Ina kasoro mengi katika fomati, kunazia tahajia ya jina kwenye lemma. Usiiache jinsi ilivyo. Tumia kwanza muda kuangalia Mwongozo wet, halafu urudi na kusafisha makala yako ya kwanza. Kipala (majadiliano) 12:19, 12 Machi 2021 (UTC)Reply

Ndugu, uwe makini: imekuwaje Dolly Mathebe ageuke kuwa Dollar Matebe? Halafu awe hai baada ya kufa miaka 17 iliyoita? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:45, 30 Oktoba 2021 (UTC)Reply
Ndugu, hubadiliki kabisa! Kila makala unakosea jina!!! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:12, 20 Septemba 2022 (UTC)Reply
Ndugu , inaweza ikawa changamoto ni divece ninayotumia maana jana niliedit makala 6 kama sio 7 .
lorenzo alvis , James F. Allan na Sarah Allen na nyingine lkn sikuwa nimekosea jina.--Frank kisamo (majadiliano) 1:42, 21 sptemba 2022 (UTC) Frank kisamo (majadiliano) 10:44, 21 Septemba 2022 (UTC)Reply
Naomba radhi kwamakosa madogo madogo yanayo jitokeza.--Frank kisamo (majadiliano) 1:46, 21 sptemba 2022 (UTC) Frank kisamo (majadiliano) 10:47, 21 Septemba 2022 (UTC)Reply
IP 41. 220. 133. 194, namba ya uzuio #2372.--Frank kisamo (majadiliano) 2:00, 21 Sptemba 2022 (UTC) Frank kisamo (majadiliano) 11:01, 21 Septemba 2022 (UTC)Reply
Angalia vizuri: ulikosea yote isipokuwa Lorenzo Alvisi ambalo umelikosea leo. Kwanza utulie kidogo. Kusahihisha kunatumaliza muda! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:32, 21 Septemba 2022 (UTC)Reply

Kupewa Muda wa kurekebisha makosa

hariri

Ndugu,ǃ salaam. Hongera kwa jitihada ya kuingeza makala katika jiografia. naomba urejee katika makala zako zote ulizo ongeza leo kwani hazina vyanzo wala muundo mzuri wa sentensi na lugha haijakaa sawa. kama hutafanya hivo kufikia saa sita usiku utafungiwa. Amani. -- Olimasy (majadiliano) Olimasy (majadiliano) 09:34, 5 Desemba 2022 (UTC)Reply

salama , nilikuwa naziweka kwenye wiki data ila sio mimi niliyezianzisha hizi makala.

Boresha Makala

hariri

Salamu, hongera kwa jitihada zako za kuanzisha makala mpya, kwa sasa unaweza kuboresha makala zako kwa kutazama marekebisho katika makala zako ambayo nimeyafanya, pia kumbuka kuweka MBEGU kulingana na aina ya makala unayofanya, kama ni makala inayomuhusu mtu, nasi weka MBEGU-MTU badala ya kuweka neno mbegu peke yake, lakini pia kumbuka kuepuka matumizi ya viungo vya ndani ambavyo haviaendani na makusudio, kwa mfano Jaji Mkuu wa kwanza Mwafrika wa Tanzania, matumizi hayo humfanya mtu kupata kitu tofauti na alichokusudia, kwa mfano hapo inaonyesha JAJI MKUU WA KWANZA MUAFRIKA,lakini mtu akifungua ndani anakutana na makala nyingine tofauti kabisa ambayo inahusu JAJI MKUU WA TANZANIA,hiyo haipendezi kwani inakwenda nje ya lengo la mtu anetaka kujifunza, pia ukiona unachotaka kukiweka hakipo, basi kiache kabisa,pia kumbuka kuingia katika ukurasa wamabadiliko ya karibuni ili kuona makala nyingine zinavyoboreshwa,Amani Sana Idd ninga (majadiliano) 08:12, 25 Januari 2023 (UTC)Reply

salamu , Asante kwa maboresho uliyoyafanya kwenye makala zangu .Nimekuelewa na nitafanya kama ulivyonishauri . Amani sana Frank kisamo (majadiliano) 11:51, 25 Januari 2023 (UTC)Reply

Kuhusu DATABOX

hariri

Salamu,naona umekuwa ukiongeza DataBox katika makala na Databox hiyo imekuwa kionyesha taarifa ambazo hazifanani na mfumo wa Kiswahili,mfano Jinsia katika DATABOX hizo inaonyesha MUME badala ya Mwanaume na kazi zinakuwa katika majina ya Kiingereza,tazama hiyo, inakuwa siyo maboreshe sahihi ya kilugha,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 14:46, 2 Februari 2023 (UTC)Reply

salamu , Nimekuwa nikiongeza Databox ilikuongeza taarifa na picha kwenye makala , hii ni baada ya kufundishwa hivyo sina uelewa mkubwa kwenye wikidata ndio maana hizo taarifa za Mume badala ya mwanaume nashindwa kuzifanyia kazi . OMBI kama ratiba yako itaruhu basi naomba tupange muda unipitishe kwenye hilo , lakini pia naedit tu databox kwasababu napenda kuchangia wikipedia ya kiswahili katika kuongeza Taarifa na kujifunza pia . Amani sana . Frank kisamo (majadiliano) 15:23, 2 Februari 2023 (UTC)Reply
Samahani kwa kuingilia mazungumzo haya, kwanza kabisa pongezi sana Frank kisamo kwa jitihada zako za kutaka kufanya kila makala walau iwe na jedwali la taarifa, lakini pia naungana na Idd ninga kuwa mengi ya majedwali hayo yanakua hayana taarifa fasaha au kiswahili kizuri cha kuendana na mkala husika, hivyo kwa ushauri ni bora uwe unatumia njia ya kawaida kutengeneza majedwali hayo badala ya kuyavuta kutoka Wikidata kwa kutumia "databox", au nenda kwenye taarifa za makala husika huko Wikidata halafu jaribu kubadilisha kiswahili kiwe kizuri hatimaye ndio uzivute taarifa hizo kwenye wikipedia ya kiswahili kwa kutumia "databox".
Asante amani iwe nasi sote Anuary Rajabu (majadiliano) 16:53, 2 Februari 2023 (UTC)Reply

Tafsiri ya Kompyuta

hariri

Salamu, naona umetumia tafsiri ya mashine katika makala hii hapa ya https://sw.wikipedia.org/wiki/Abadon_(wrestler) , kitu ambacho hakitakiwa, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 08:01, 13 Februari 2023 (UTC)Reply

Taarifa ya kukuzuia!

Ndugu, imenibidi kukuzuia kwa sababu zinazotajwa chini. Wakati unapokuwa umezuiwa huwezi kuhariri isipokuwa penye huu ukurasa wako wa majadiliano. Unaweza kunijibu kwa kutumia “Email this user”.

Sababu ni kuwa umeingiza matini iliyopatikana kwa njia ya tafsiri ya kompyuta ikiwa na kasoro nzito ya lugha. Umearifiwa kwamba ni marufuku kumwaga matokeo ya google translate katika makala zetu. Wachangiaji wanaopuuza utaratibu huu wanasababisha hasara kubwa kwa Wikipedia yetu na kuwapa wengine kazi kubwa mno ya kusafisha makosa yao.

Bila shaka una nia nzuri kuchangia katika Wikipedia. Tutafurahi kushirikiana nawe lakini ni lazima ufuate utaratibu. Kazi yetu kama wakabidhi ni kulinda mradi huu.

Ukiwa tayari kufuata utaratibu pamoja na kupitia upya matini ulizozileta tayari, naomba uwasiliane nami kwa kufungua ukurasa wangu (bofya jina langu chini) na kuniandikia baruapepe kwa kubofya “Email this user” upande wa kushoto. Hapo nitaweza kukuruhusu tena. Hapo lazima uwezeshe njia kwa kufuata maelezo katika Wikipedia:Email.

Masahihisho

hariri

Ndugu, juhudi zako zinaendelea, lakini angalia pia makala zako zinavyosahihishwa na wakabidhi. Mara nyingi makosa ni yaleyale... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:56, 18 Februari 2023 (UTC)Reply