Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!

Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.

Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na n) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.

Kwa mawili matatu labda tazama:

Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.

Ujue miiko:

Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!


Welcome to Kiswahili Wikipedia!

We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:

  • do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
  • nor copied texts/images from other webs to this site!
  • do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.

As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.

Usihangaike kuondoa "y" katika kitenzi "kuonyesha": kamusi zote zinakubali kwamba ni sahihi, hata kama shuleni wanapinga. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:52, 12 Julai 2019 (UTC)Reply

Tangazo hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo Wa Kimataifa Wa Mwenendo Na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuainisha vitu vya msingi vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa  uchangiaji (uhariri) wa Wikipedia na pale wanawikipedia wanapowasiliana kwenye Wikipedia au ana kwa ana katika warsha na mikutano ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kukithiri kwa baadhi ya Wanawikimedia kukumbana kufanyiwa unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na  Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Hivyo, wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huo Hapana baada ya kuusoma mwongozo huo unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 15 April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Dar es Salaam ili tuweze kujadiliana na kubadilishana uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla na miradi waliyoitekeleza tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi AMtavangu (WMF) (majadiliano) 21:46, 5 Aprili 2020 (UTC)Reply

Mwaliko wa kutoa maoni yako kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Nidhamu hariri

Habari ndugu Mwanawikipedia!

Mimi ni mwezeshaji wa mradi uitwao Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Ni mradi mchanga/mpya ambao Shirika la Wikimedia Foundation linanuia kuuanzisha endapo wadau wataona ni mradi unaofaa na kuunga mkono wazo hilo. Nakukaribisha usome mwongozo huo na kisha utoe maoni yako kwa kujibu maswali yote au baadhi yake kwa yale utakayopenda kuyatolea maoni HAPA

Taarifa zaidi kuhusu Mwongozo wa Kimataifa wa Nidhamu na Mwenendo

Shirika la Wikimedia Foundation lina mpango wa kuanzisha Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili. Lengo la mwongozo huo ni kujaribu kuoanisha vitu vya msingi vya kimwongozo vinavyopatikana katika miongozo midogo midogo iliyopo tayari katika kila jamii husika (mfano katika Jumuiya yetu hii ya wahariri wa Wikipedia ya Kiswahili). Lengo hasa la mwongozo huu ni kujaribu kutengeneza mazingira ambayo wanawikipedia wote duniani watakuwa na uelewa wa pamoja juu ya vitu vya msingi kuhusu nini kinakubalika na kipi hakikubaliki wakati wa uchangiaji (uhariri) au utumiaji wa Wikipedia, na pia pale wanawikipedia wanapowasiliana ndani ya tovuti ya Wikipedia yenyewe au wanapokutana ana kwa ana katika warsha na mikutano mbalimbali ya Wanawikipedia. Wazo hilo limekuja baada kutokea kwa baadhi ya matukio kwa baadhi ya Wanawikimedia anbapo katika tafiti iliyofanywa mwaka 2015 , ilionekana baadhi ya Wanawikimedia walikuwa wakikumbana na unyanyasaji wa kitabia (mfano matusi, kuitana majina yasiyofaa, kutishiana n.k) na Wanawikimedia wenzao, hivyo kuwakatisha tamaa ya kuendelea kuchangia katika miradi ya Wikimedia.Wewe kama mdau muhimu katika miradi ya Wikimedia Foundation, unakaribishwa ku soma zaidi kuhusu mwongozo huona unaweza ku toa maoni yako Hapa kabla ya tar 29th April 2020.

Mwaliko wa kujiunga na kundi la Wahariri wa Wikipedia

Nakukaribisha ujiunge na kundi la Wahariri wa Wikipedia kutoka Tanzania (Dar es Salaam) ili tuweze kujadiliana na kubadilishana mawazo, uzoefu na mambo kadha wa kadha kuhusu Uhariri wa Wikipedia na miradi mingine yake ya Wikimedia Foundation. Iwapo utapenda kujiunga, usisite kuwasiliana nasi kupitia wikitzagroup@gmail.com, na kwa taarifa zaidi kuhusu kundi la Wahariri wa Wikipedia wa hapa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuhusu miradi waliyoifanya tayari, unaweza tembelea hapa ukurasa wao wa meta uitwao Wikimedia Community User Group Tanzania au pia katika Facebook kwa jila la Wikimedia Tanzania.

Ndimi Mtavangu19:09, 18 Aprili 2020 (UTC)Reply

Tafsiri hariri

Ndugu, nakukumbusha usitumie vifaa vya kutafsiria kielektroni kwa sababu matokeo hayaeleweki. Siwezi kupoteza muda mwingi hivi kurakebisha sentensi ngumu zisizoeleweka. Punguza mwendo wako: afadhali ukurasa mmoja mzuri kuliko 10 ngumu mno. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:29, 11 Machi 2021 (UTC)Reply

Kwa kuwa unaendelea kuanzisha makala zisizoeleweka nakuzuia kwa siku tatu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:54, 18 Machi 2021 (UTC)Reply
samahani nawezaje kutafsiri tofauti na tool ambayo inanipeleka moja kwa moja kutafsiri ama muongozo wowote ambao utaelekeza namna bora ya utafsiri.
Natarajia na napenda kuhariri makala bora
AHSANTE Killy95 (majadiliano) 08:12, 18 Machi 2021 (UTC)Reply
Ndugu, nimetambua nia yako njema, ndiyo sababu nimekuzuia kwa siku tatu tu. Kitu kikubwa ni kwamba ukitumia hiyo tool usiiamini, ni lazima upitie mwenyewe tafsiri yake neno kwa neno kuona kama inaeleweka na maana yake. Kama sivyo, futa sentensi husika. afadhali kibaki kidogo cha kueleweka kuliko uchafu mkubwa usiomfaa mtu yeyote. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:19, 18 Machi 2021 (UTC)Reply
Shukrani kwa msaada nimeelewa nitahakiki kwa usahihi. Killy95 (majadiliano) 08:30, 18 Machi 2021 (UTC)Reply
Endelea kukakikisha kwamba makala zako zieleweke vizuri kwa Kiswahili. Unavyojua, tafsiri ya kompyuta haisaidii sana. Endelea pia kuangalia kama pengine ninarekebisha michango yako ili uzidi kukomaa. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:31, 16 Aprili 2021 (UTC)Reply

Miji ya Uganda hariri

Tafadhali, chini ya makala za aina hii, bandika kama ifuatavyo: ==Marejeo== {{reflist}} {{mbegu-jio-Uganda}} [[Jamii:Miji ya Uganda]] [[Jamii:Wilaya ya Amuru]] [[Jamii:Africa Wiki Challenge 2021 in Tanzania]] Asante sana kwa ushirikiano. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:49, 23 Julai 2021 (UTC)Reply

Bila shaka, baadaye badilisha jina la wilaya! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:52, 23 Julai 2021 (UTC)Reply

Umesimamishwa hariri

Ndugu umeanza kuleta makala ambako naona unatumia tena tafsiri ya kompyuta bila masahihisho. (Iubaltiana). Haikubaliki na umeshaambiwa mara kadhaa. Nimekubana sasa. Unaweza kuwasilianina nami kwa kutumia email. Tukielewana nitakuruhusu tena. Tafadhali niambie ni nafasi gani ambako mlipatana kutafsiri makala juu ya Tunisia. Kwa bahati mbaya hamjaandaliwa ipasavyo, nimeona makala nyingi zenye kasoro nzito. Kipala (majadiliano) 14:28, 30 Julai 2021 (UTC)Reply

Habari Samahani wakati naifungua kabla ya kuanza kuipitia kifaa kilileta shida. Na nikasahau kama niliishia wapi hivyo nikaendelea. Hivyo kwa tafsiri iliyo haririwa inaonesha ni mtu lakini uhalisia ni mji.

Ahsante Killy95 (majadiliano) 14:38, 30 Julai 2021 (UTC)Reply

Nimepitilia makala kadhaa ulizotunga katika siku zilizopita. Picha ninayopata ni hii: umejaribu kuunda makala nyingi iwezekanavyo bila kujali maudhui. Matokeo yake ni makala ambazo mara nyingi hazina maana kabisa au kidogo tu, pamoja na makala nyingi za kushangaza na kumpotosha msomaji. Sababu kuu ni a) mara nyingi ulitumia tafsiri ya google bila kujali, yaani bila kuangalia kama matokeo yana maana kwa Kiswahili b) makala nyingine ulifupisha sana sijui kwa sababu hujaelewa Kiingereza au ulitaka kuendelea haraka (kufupisha ni sawa ila tu lazima maana fulani ibaki!) yaani mwishoni tuna habari fupi sana, haitaji chochote kuhusu mabaki ya kihistoria lakini unaweka yote katika jamii ya "maeneo ya kiakolojia"????
Jebil National Park (jina si Kiswahili, wala si jina lenyewe ya kwao): haina maudhui ya akiolojia, haiko kwenye jamii yake ya mbuga wa kitaifa
Aeliae: Unatumia marejeo bila kujali, rejeo lililopo ni kuhusu hali yake kuwa dayosisi ya zamani, lakini habari hii hujatafsiri;
Jebil National Park , Sousse, Aeliae, Theveste, Thibilis (bila chanzo chochote!), Timgad: maelezo yoyote kuhusu magofu au mabaki ya kihistoria hujatafsiri, lakini unapanga yote katika jamii ya maeneo ya akiolojia??
Rufiniana, Raqqada, Ausafa, Aïn Doura Baths (??), Ad_Turres_(Byzacena), Thiava, Numidia, Tigisis (Mauretania), Timgad: umetumia tafsiri ya google bila kujali matokeo; lugha haieleweki
Tatizo si ile makala moja niliyotaja juu. Umerudia mara nyingi, sijui nitapata ngapi nikiangalia nyuma zaidi. Ukiwa na hoja jinsi ya kurekebisha mambo, tafadhali niandikie kwenye ukurasa wangu. Kipala (majadiliano) 22:47, 30 Julai 2021 (UTC)Reply
Mbona hubadiliki? Nakusimamisha tena. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:00, 17 Machi 2022 (UTC)Reply