Makrina Mdogo

Makrina Mdogo (Kaisarea wa Kapadokia 330 hivi - Ponto 369) alikuwa mwanamke mmonaki, binti Bazili Mzee na Emelia wa Kaisarea. Alipewa jina hilo kwa heshima ya bibi yake, Makrina Mkubwa, ambaye anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na wajukuu wengine kama Bazili Mkuu, Gregori wa Nisa na Petro wa Sebaste.

Makrina Mdogo.

Mwenyewe pia anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali kama mtakatifu bikira.

Sikukuu yake ni tarehe 19 Julai[1].

Sala yakeEdit

Ee Bwana, wewe umetuondolea hofu ya kifo.

Mwisho wa maisha yetu hapa umeufanya mwanzo wa uzima wa kweli.

Kwa kitambo tu utaacha miili yetu ilale usingizi, halafu kwa tarumbeta ya mwisho utaiamsha kutoka usingizini.

Wewe unaukabidhi udongo ukutunzie udongo wako huu ulioufinyanga kwa mikono yako; nawe utauchukua tena na kutoka fungu la kufa, lisilo na muundo, utaugeuza kuwa na uzuri usiokufa.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Kwa KiswahiliEdit

  • PADRE FRIDOLIN, Maisha ya Mtakatifu Makrina - ed. N.M.P. - Ndanda

Kwa lugha nyingineEdit

  • A. M. Silvas, Macrina the Younger. Philosopher of God, Turnhout, 2008, Brepols Publishers, ISBN 978-2-503-52390-3
  • Nester, Marie Yaroshak. We Are God's People, God With Us Publications, 2004, p. 99.
  • Burrus, V. "Macrina's Tattoo," in D. B. Martin and P. Cox Miller (eds), The Cultural Turn in Late Ancient Studies: Gender, Asceticism, and Historiography (Durham (NC), 2005), 103-116.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.