Petro wa Sebaste
Petro wa Sebaste (340 hivi – 26 Machi 391) alikuwa askofu wa mji huo, Sebaste katika Armenia Ndogo.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, sawa na kaka zake Basili Mkuu, Gregori wa Nisa, na dada yao Makrina Mdogo, ambao walimuathiri sana tangu utotoni.
Maisha
haririBibi yake alikuwa Makrina Mkubwa, aliyefundishwa na Gregori Mtendamiujiza. Wazazi wake, Basili Mzee na Emmelia wa Kaisarea ya Kapadokia, walifukuzwa na kaisari Galerius Maximian kwa sababu ya imani hiyo, wakahamia jangwa la Ponto.
Mtoto wa kumi na wa mwisho, Petro alilelewa na kuelekezwa kwenye maisha ya Kiroho na Makrina Mdogo[2].
Akiachana na masomo ya elimudunia, Petro alijitosa katika kutafakari Biblia.
Kidogo tu baada ya Basili kufanywa askofu wa Caesarea, Petro alipewa naye upadrisho, lakini baadaye akatawa tena kama mkaapweke, akawasaidia mama na dada kuanzisha monasteri nyumbani mwao baada ya kifo cha baba. Mwenyewe aliongoza jumuia ya kiume na Makrina ile ya kike. [3]
Ponto na Kapadokia zilipopatwa na njaa kali, alionyesha ukarimu wake kwa kutoa mali zote za monasteri na kila alichokipata awasaidie umati uliomkimbilia.
Mwaka 380 hivi aliteuliwa kuwa askofu wa Sebaste akaunga mkono juhudi za kaka zake dhidi ya Uario. Vilevile katika uchungaji alimfuata Basili.
Mwaka 381 alishiriki Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli.[4]
Kwa ombi lake, Gregori wa Nisa aliandika vitabu vyake maarufu, Against Eunomius, Treatise on the Work of the Six Days na On the Endowment of Man.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Butler, Alban. "St. Peter of Sebaste, Bishop and Confessor", The Lives of the Saints, Vol.I, 1866
- ↑ Kirsch, Johann Peter. "St. Peter of Sebaste." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 16 March 2015
- ↑ "St Peter the Bishop of Sebaste, in Armenia", Orthodox Church in America
- PADRE FRIDOLIN, Maisha ya Mtakatifu Makrina - ed. N.M.P. - Ndanda
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |