'

Mama Cax
Mama Cax akiwa kwenye onyesho la mitindo.
AmezaliwaNovemba 20, 1989
AmefarikiDesemba 16, 2019
Kazi yakemwanamitindo na mwanaharakati wa haki za walemavu kutoka Marekani


Cacsmy Brutus (anayejulikana kama Mama Cax[1]; Novemba 20, 1989 - Desemba 16, 2019) alikuwa mwanamitindo na mwanaharakati wa haki za walemavu kutoka Marekani-Haiti.[2][3]

Maisha

hariri

Cacsmy alizaliwa Brooklyn, New York City, mnamo Novemba 20, 1989. Alilelewa Haiti, na alipokuwa na umri wa miaka 14, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kansa ya mifupa (kwa Kiingereza: Osteosarcoma) na kansa ya mapafu; madaktari walimpa wiki tatu za kuishi. Miaka miwili baadaye, aliwekewa nyonga ambayo haikufaulu, na kusababisha kukatwa kwa mguu wake wa kulia.[4] Baadaye alisema kwamba ilichukua miaka kadhaa kurejesha ujasiri wake na kwamba alificha mguu wake bandia kwa miaka kadhaa.

Alipata digrii ya bachelor na shahada ya uzamili kuhusu mahusiano ya kimataifa.[5] Akiwa na umri wa miaka 18, Cax alijifunza kucheza mpira wa kikapu wa viti vya magurudumu.

Mnamo Septemba 15, 2016 Cax alialikwa kwenye Ikulu ya Marekani ili kushiriki katika onyesho la mitindo lililoandaliwa na Barack Obama na Michelle Obama. Wakati huo, alikuwa akifanya kazi katika ofisi ya Meya wa Jiji la New York.[6]

Mwaka wa 2017, Cax alionekana katika tangazo lake la kwanza la kibiashara, na punde alisaini na wakala wa urembo wa JAG Models huko New York. Miongoni mwa maonyesho yake pia alitembea kwenye maonyesho ya urembo ya Chromat na Fenty Beauty inayomilikiwa na Rihanna.[7] Kazi yake ya baadaye ya kibiashara ilijumuisha kampeni za matangazo ya Tommy Hilfiger na Sephora.

Mnamo 2018, alitembea kwenye New York Fashion Week akivalia vazi la kuogelea lililoundwa na Becca McCharen, ambaye alikuwa na shauku kubadilisha viwango vya urembo. Mwaka huohuo, alitokea kwenye jalada la Teen Vogue akiwa na Jillian Mercado na Chelsea Werner.[8]

Mnamo 2019, sura ya Cax ilitumika kama chapa ya kampuni ya Olay kwa kampeni ya uuzaji ya mafuta ya jua. Mnamo Oktoba 2019, Cax alitangaza kuwa atashiriki kwenye New York Marathon kwa kiti cha magurudumu.

Akiwa Uingereza mnamo Desemba 2019, Cax alilazwa Royal London Hospital kwa maumivu makali ya tumbo na kuganda kwa damu kwenye mapafu; alifariki hospitalini hapo mnamo Desemba 16, 2019.

Marejeo

hariri
  1. "Model-activist Mama Cax dead at 30". Page Six Style (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-20.
  2. "Model-The Trailblazing Model Mama Cax Has Died at 30". Vogue (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-20.
  3. "Boundary-breaking model Mama Cax dies at 30". The Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-20.
  4. "Mama Cax on Her Amputation, Beauty, and Body Positivity: "I Felt Pride, and That Changed Everything"30". Glamour Logo (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-05-03.
  5. "About". Mamacax.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2015-02-04.
  6. "Model-Activist Mama Cax on Traveling with a DisabilityInterview". Here Magazine (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "No One's Gonna Miss The Victoria's Secret Fashion Show". Buzz Feed News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-11-26.
  8. "This Model-Activist and Amputee's Runway Walk Just Lit Up the Chromat Show". Vogue (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-09-7. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mama Cax kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.