Maria Teresa Goretti (Corinaldo, Ancona, Italia, 16 Oktoba 1890 - Nettuno, Lazio, 6 Julai 1902) alikuwa bikira Mkristo ambaye, baada ya kupitia utoto katika ufukara akimsaidia mama yake mjane katika shughuli za nyumbani na kudumu katika sala, alikataa mfululizo kuzini na jirani yake Alessandro Serenelli, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa kifaa cha chuma[1].

Sanamu ya Mt. Maria Goretti katika mavazi ya mkulima akishika maua na kisu.
Nyumba alimoishi na kupigwa Maria Goretti.

Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni dhambi!"

Kabla hajafa hospitalini, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye mbinguni.

Baada ya miaka mitatu gerezani, Alessandro aliongoka na alipotoka alikwenda kuomba msamaha wa mama wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea ekaristi pamoja.

Halafu akaishi utawani kwa Wakapuchini wa Macerata hadi alipofariki mwaka 1970.

Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Aprili 1947 na kuwa mtakatifu tarehe 24 Juni 1950, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 6 Julai ya kila mwaka[2].

Tazama pia

hariri

Filamu juu yake

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Beatificationis seu declarationis martyrii Mariae Goretti, Roma, 1938-1939 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mwenye heri).
  • Compendium vitae virtutum ac miracolorum Beatae Mariae Theresiae Goretti, Typis Polyglottis Vaticani, 1950 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mtakatifu).
  • A proposito di Maria Goretti: santità e canonizzazioni: atti della Commissione di studio istituita dalla Congregazione per le cause dei santi il 5 febbraio 1985, Città del Vaticano, Libreria Editrice Vaticana, 1986.
  • Giovanni Alberti, Maria Goretti, Città Nuova Editrice, 1980. ISBN 88-8386-150-7.
  • Giordano Bruno Guerri, Povera santa, povero assassino. La vera storia di Maria Goretti, Mondadori, Milano, 1985 - toleo jipya lililorekebishwa na kuongezewa Bompiani, Milano, 2008.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.