Marina wa Omura
Marina wa Omura (alifariki Nagasaki, 11 Novemba 1634) alikuwa bikira wa Utawa wa Tatu wa Mt. Dominiko nchini Japani.
Baada ya kufungwa gerezani na kudhihakiwa kwa ubikira wake, alibakwa hadharani halafu akachomwa moto taratibu akiwa hai akawa hivyo mmojawapo kati ya Wakristo wa Kanisa Katoliki waliofia dini nchini humo[1].
Anaheshimiwa kama mtakatifu pamoja na Lorenzo Ruiz na wenzao waliotangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa wenye heri tarehe 18 Februari 1981 halafu watakatifu tarehe 18 Oktoba 1987.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 28 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe ya kifodini chake[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Lorenzo de Manila, The Proto-Martyr of The Philippines and his Companions - Fr. Fidel Villarroel, O.P., 1988
- Constantino Alvares, Jose Garcia, Pedro Tejero, Witnesses of the faith in the Orient: Dominican Martyrs of Japan, China, and Vietnam, Manila, Life Today Publications, 1989, ISBN 971-8596-03-8
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |