Marselino na Petro
Marselino na Petro ni Wakristo wa karne ya 3 waliouawa mwaka 304 kwa ajili ya imani yao mjini Roma[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Maisha
haririKuhusu maisha yao, hatuna habari nyingi za hakika. Marselino alikuwa padri, na Petro mzinguaji. Wote wawili waliuawa kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Kaisari Diokletian dhidi ya Wakristo wa Dola la Roma.
Simulizi la kifodini chao la Papa Damas I ndilo chanzo cha kale zaidi juu yao. Damas alieleza kwamba alipata habari kutoka kwa muuaji wao ambaye baadaye alijiunga na Kanisa[3][4]
Kwake tumepata kujua kwamba walipopelekwa kwenye vichaka vya miiba ili kuuawa, walilazimishwa kujichimbia makaburi yao, ili maiti wasionekane na yeyote, lakini Lusila alifaulu kuwazika kwa heshima mjini kwenye barabara inayoitwa Labicana, ambapo baadaye lilijengwa basilika maarufu[5].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Alban Butler, Kathleen Jones, Paul Burns, Butler's Lives of the Saints (Continuum International Publishing Group, 1997), 14.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ Amore, Agostino (5 Nov 2008). "Santi Marcellino e Pietro". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo Januari 9, 2009.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ ? (n.d.). "SS. Marcellinus and Peter". Eternal Word Television Network. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-10-12. Iliwekwa mnamo Januari 9, 2009.
{{cite web}}
:|author=
has numeric name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/27550
Vyanzo
hariri- Catholic Online
- Anna Jameson: Sacred and Legendary Art Ilihifadhiwa 10 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
- Saints of 2 June Ilihifadhiwa 6 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |