Memphis, Misri

(Elekezwa kutoka Memphis, Egypt)

Memphis ilikuwa mji mkuu wa Misri ya Kaskazini, na baadaye pia ya Misri ya Kale yote kuanzia maungano ya Misri ya Kaskazini na Misri ya Kusini chini ya Farao Menes hadi karibu mwaka 2200 KK. Baadaye ilirudi tena kama mji mkuu wakati wa Ufalme Mpya wa Misri. [1] Kilikuwa kitovu cha utawala hadi utawala wa Kiroma juu ya Misri.[2] [3]

Mabaki ya ukumbi wa nguzo, Memphis ya Kale (leo Mit Rahineh)

Jina lake la zamani kwa Kimisri lilikuwa Ineb Hedj ("Kuta Nyeupe"). Jina "Memphis" ( Μέμφις ) lilitungwa na Wagiriki waliojaribu kutamka jina la piramidi ya Pepi I (nasaba ya 6), ambayo ilikuwa Men-nefer, [4] likawa Menfe katika matamshi ya kawaida.

Miji ya kisasa ya Mit Rahina, Dahshur, Saqqara, Abusir, Abu Gorab, na Zawyet el'Aryan, kusini mwa Kairo, yote iko ndani ya mipaka ya kiutawala ya Memphis ya kihistoria ( 29°50′58.8″N, 31°15′15.4″E ).

Memphis pia ilijulikana katika Misri ya Kale kama Ankh Tawy ("Inayoshika nchi zote mbili") kwa sababu ya nafasi ya kimkakati ya mji kati ya Misri ya kusini na Misri ya kaskazini.

Maghofu ya Memphis yako km 20 kusini mwa Kairo, kwenye ukingo wa magharibi wa mto Nile.

Hiroglifi huko Memphis na sanamu ya Ramses II nyuma.

Katika Biblia, Memphis inaitwa Moph au Noph.

Maghofu yake pamoja na maeneo mapana ya makaburi ya enzi za Misri ya Kale, pamoja na Sakara na Pirmidi za Gizeh, yamepokelewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO[5].

Marejeo hariri

  1. Katheryn A. Bard, Encyclopedia of the Archaeology of Ancient Egypt, Routledge 1999, p.694
  2. Lynn Meskell, Private Life in New Kingdom Egypt, Princeton University Press 2002, p.34
  3. Ian Shaw, The Oxford History of Ancient Egypt, Oxford University Press 2003, p.279
  4. Bridget McDermott, Decoding Egyptian Hieroglyphs: How to Read the Secret Language of the Pharaohs, Chronicle Books 2001, p.130
  5. Memphis and its Necropolis – the Pyramid Fields from Giza to Dahshur, tovuti ya Unesco, iliangaliwa Machi 2021

Vyanzo hariri

  • Baines & Malek Atlas ya Utamaduni ya Misri ya Kale, 2000 

Majiranukta hariri

Coordinates: 29°50′40.8″N, 31°15′3.3″E

  Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Memphis, Misri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.