Method Kilaini (amezaliwa Katoma, Bukoba, 30 Machi 1948) ni askofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania aliyewahi kuhudumia kama askofu msaidizi kwanza Jimbo Kuu la Dar es Salaam, halafu Jimbo la Bukoba hadi Januari 2024.

Maisha hariri

Askofu Kilaini alipewa upadrisho kama padre wa jimbo la Bukoba jijini Roma mwaka 1972 na Kardinali Agnelo Rossi baada ya kupata shahada ya pili ya teolojia huko Roma.

Baada ya kurudi nyumbani Bukoba, Tanzania, alifanya kazi parokiani, baadaye alikuwa mhazini msaidizi wa jimbo.

Kati ya mwaka 1978 hadi 1985 alifundisha Historia ya Kanisa katika Seminari Kuu ya Ntungamo.

Mwaka 1985 alirudi Roma na kupata shahada ya udaktari wa tauhidi katika Historia ya Kanisa kutoka chuo Kikuu cha Gregoriana mwaka 1990.

Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.

Kuanzia mwaka 2000 alikuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam hadi mwaka 2009 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

Huko Dar es Salaam Askofu Kilaini anakumbukwa kwa kuratibu majengo mengi yaliyopo hapo makao makuu ya maaskofu Kurasini na kuongeza viwanja vya kanisa. Vile vile alishiriki sana kuleta maelewano kati ya viongozi wa dini mbalimbali. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa tume ya Kikristo ya huduma za jamii mwaka 1992 (CSSC), vilevile wa tume ya amani ya viongozi wa dini mwaka 1994.

Jimboni Dar es Salaam alisaidia kuanzisha Television Tumaini na kuimarisha Jumuiya Ndogondogo za Kikristo.

Kule Bukoba alisaidia kukamilisha ukarabati wa Kanisa Kuu la jimbo na kuratibu kuhamisha mwili wa Laurean Kardinali Rugambwa. Alisaidia vilevile kuanzisha Radio Mbiu akishirikiana na Radio Maria.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.