Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam
(Elekezwa kutoka Jimbo Kuu la Dar es Salaam)
Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam (kwa Kilatini Archidioecesis Daressalaamensis) ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Chini yake kuna kanda ya Kanisa yenye majimbo yafuatayo: Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mahenge na Ifakara.
Askofu mkuu wake ni Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, O.F.M.Cap..
Historia
hariri- 16 Novemba 1887: Kuanzishwa kwa Apostolic Prefecture ya Dar-es-Salaam kutokana na Apostolic Vicariate ya Nairobi
- 15 Septemba 1902: Kupandishwa hadhi kuwa Apostolic Vicariate ya Dar-es-Salaam
- 25 Machi 1953: Kufanywa dayosisi (jimbo kuu)
Uongozi
hariri- Maaskofu Wakuu wa Dar-es-Salaam
- Yuda Thaddeus Ruwa'ichi (tangu 2019)
- Kardinali Polycarp Pengo (1992 - 2019)
- Kardinali Laurean Rugambwa (1968 – 1992)
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1953 – 1968)
- Vicar Apostolic wa Dar-es-Salaam
- Edgar Aristide Maranta OFMCap (1930 – 1953)
- Joseph Gabriel Zelger OFMCap (1923 – 1929)
- Thomas Spreiter OSB (1906 – 1920)
- Cassian Spiß OSB (1902 – 1905)
- Prefect Apostolic wa Dar-es-Salaam
- Padri Maurus Hartmann OSB (1894 – 1902)
- Padri Bonifatius Fleschutz OSB (1887 – 1891)
Takwimu
haririEneo la jimbo lina kilometa mraba 40,000 hivi, ambapo kati ya wakazi 5,798,760 (2017) Wakatoliki ni 1,724,371 (sawa na 29.7%).
Parokia ziko 109, zikihudumiwa na mapadri 285 (81 wanajimbo na 204 watawa), watawa wanaume wasio mapadri ni 268 na wanawake ni 669.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jimbo Kuu la Dar-es-Salaam kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |