Mfereji wa Msumbiji


Mfereji wa Msumbiji (kwa Kiingereza Mozambique Channel, kwa Kifaransa Canal du Mozambique, kwa Kimadagaska: Lakandranon'i Mozambika, kwa Kireno: Canal de Moçambique) ni sehemu ya Bahari Hindi iliyopo kati ya kisiwa cha Madagaska na bara la Afrika, hasa nchi ya Msumbiji.

Mahali pa Mfereji wa Msumbiji

Sehemu yake nyembamba yenye upana wa kilomita 460 iko kati ya Angoche, Msumbiji na Tambohorano, Madagaska. Urefu wake ni takribani km 1,600. Maji yake yanafikia kina cha mita 3,292 .

Mfereji huu unapitiwa na mkondo wa bahari unaopeleka maji ya vuguvugu hadi pwani ya Afrika Kusini.

Visiwa katika Mfereji wa MsumbijiEdit

KomoriEdit

Maeneo ya ng’ambo la UfaransaEdit

Iles Eparses (Visiwa vilivyotawanyika)Edit

MadagaskaEdit

  • Nosy Be
  • Nosy Hara
  • Nosy Mitsio

MsumbijiEdit

Viungo vya njeEdit


Majiranukta kwenye ramani: 18°S 41°E / 18°S 41°E / -18; 41