Milima ya Mhandu iko magharibi mwa Tanzania katika Mkoa wa Shinyanga. Milima hii inapatikana katika Wilaya ya Kahama Vijijini katika kata za Segese, Chela na Bulige katika kijiji cha Mwaningi. Milima hii inaendelea kuelekea Mkoa wa Geita na Mwanza.

Kilele cha juu kiko mita 1,481 juu ya usawa wa bahari.

Masimulizi ya wenyeji

hariri

Katika milima ya Mhandu kuna chemchemi zisizokauka katika eneo la Igobole (unaitwa kasela ya Fufumo), hii huaminika kuwa hapo zamani watu walikuwa wanapotelea pale kimiujiza endapo wakiwa na damu mbaya.

Nfufumo ni jina la mtemi aliyekuwa anapatikana eneo hilo; baada ya kufariki miaka mingi iliyopita ndipo hiyo chemchemi ya maporomoko ya maji yakatokea na hadi leo hii yapo.

Maeneo mengine ya maajabu katika milima ya Mhandu ni Kasela ya Chela, kasela ya Mwankumbi (zote chemchemi zisizokauka) ukithubutu kupaharibu majitu ya ajabu hutokea.

Wakazi na historia yao

hariri

Walongo (kwa Kisukuma: Bhalongo) ndio wakazi asilia wa eneo la Mhandu kabla ya uvamizi wa kabila la Wasukuma kutoka Mwanza.

Balongo walijishughulisha na ufuaji wa vyuma, kilimo pamoja na biashara ya pembe za ndovu na vyuma walibadilishana na Wanyamwezi, Wasumbwa, Wasukuma, Wasubi, Wakamba au Bhaloha ambao nao ni wakazi wa eneo hilo na pia ndio watawala katika eneo, pia walibadilishana na Wazinza kutoka Sengerema.

Dini ya Bhaloha ni kuabudu mungu wao aitwae Lyubha au Welelo

Tazama pia

hariri