Walongo
Walongo ni kundi dogo la kabila la Wahaya, mchanganyiko na Wanyambo, Wanyankole, Wahima na Watutsi, linaloshabihiana sana na Wazinza. Lugha yao ya Kilongo ni lahaja ya Kihaya.
Wanakaa katika Mkoa wa Geita. Walihamia Geita na Sengerema miaka mingi iliyopita, kutokana na vita, mauaji ya mapacha, utawala wa mabavu na uchawi uliokuwa ukiendelea katika maeneo yao wakati huo.
Omulongo (ikimaanisha pacha) na Abalongo (ikimaanisha mapacha) pamoja na wazazi wao na ndugu zao baadhi waliamua kuhama kwenda sehemu salama ambapo waliita (longooka), na hapo ndipo ikawa mwanzo wa jamii ya Walongo katika mkoa wa Geita na wilaya ya Sengerema.
Kuhama kwao walipitia ziwani na kutokezea sehemu ambayo panaitwa Kamuhanga (ikimaanisha Bondeni "Creator") au kwa Kinyankole Nyamuhanga, walipita pia kwenye mlima mrefu uliokuwa unawaua sana kutokana na urefu wake ambao walikuwa wanauita "Akabanga Keita Abantu" ikimaanisha mlima unaoua watu na hapo ndio ikawa mwanzo wa jina la Geita. Jina Geita lilitokana na kushindwa Wazungu kulitamka neno "Akabanga Keita Abantu" wakachukua neno "Keita" nalo pia walilitamka kama "Geita".
Wengine walifika hadi kaskazini mwa mkoa wa Kigoma ambako kuna ukoo wa Kiha ambao wanaitwa Wabanga au Abhabhanga: hao ni Walongo waliohamia Kigoma kutokea Geita, wakapita Biharamulo, hadi Kakonko Kigoma na wamekuwa wakifuata mila zao za Walongo hadi sasa ingawa kwa sasa wamechanganyika na Waha.
Wengine walipitia ziwani wakitokezea sehemu panaitwa Akabaare (Nyakabaare) ikimaanisha jiwe jeusi linalonyonya sumu ya nyoka, na wengine walipitia sehemu kama Muleba, Biharamulo, Chato hadi Geita mjini na wengine Muleba, Biharamulo, Kahama na mwisho wakakaa Msalala (Geita).
Kazi walizokuwa wakizifanya ni uvuvi, ufugaji, uwindaji, uhunzi wa vyuma na kilimo hasahasa cha mihogo, mpunga na ndizi.
Kwa sasa Walongo wamechanganyikana sana na Wasukuma kutokana na kuoana sana baada ya Wasukuma wengi kuhamia Geita.
Baadhi ya maeneo ya Geita yenye majina ya Kilongo
hariri- Nkome - inamaanisha ng'ombe mwenye mapembe yaliyonyooka mbele.
- Kamena - inamaanisha mwezi wa tisa.
- Lubanga au Ebbanga - inamaanisha umbali, muda au kipindi fulani katika kufikia kitu.
- Senga au Ssenga - inamaanisha shangazi.
- Bwanga au Obwanga - ikimaanisha tumbaku.
Baadhi ya majina ya kilongo
hariri- Gogomoka(Kugomoka)- ikimaanisha anaenenepa
- Mwegi- ikimaanisha mwanafunzi
- Leekwa- ikimaanisha mtoto alieachwa mkiwa
- Huuru(ehuuru)- ikimaanisha mtu mfupi mwenye umbo dogo( Dwarf)
- Bugomora(Kugomora)- ikimaanisha anaenenepesha mtu au wanyama. Au anaetatua matatizo
- Sengeka- ikimaanisha kupanga au kuweka kitu katika mpangirio mzuri
- Buguma- kuwa wa moto
- Ziba- ikimaanisha kuziba au kuzuia kitu kwa kitendo wanasema(zibye)
- Tuula- inamaanisha kukaa
- Ngoto (engoto)- ikimaanisha Shingo
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Walongo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |