Mfereji

(Elekezwa kutoka Mifereji)

Mfereji ni njia ya maji iliyotengenezwa na watu, tofauti na njia asilia za maji kama mito au maziwa.

Mfereji mdogo wa umwagiliaji nchini Uswisi

Kuna aina mbili za mifereji:

Historia

hariri

Mifereji ya kwanza inayojulikana ilitengenezwa zamani za Mesopotamia ya Kale, Misri ya Kale au Uhindi ya Kale kwa umwagiliaji.

Mnamo mwaka 2300 KK mfalme Pepi I aliamuru mfereji kuchimbwa kama njia ya usafiri wa kuepukana na maporomoko ya mto Naili karibu na Aswan.

Mfalme Necho II wa Misri alianzisha njia ya maji ya kwanza kati ya Mediteranea na Bahari ya Shamu kwa kuchimba mfereji kati ya mto Naili na Bahari ya Shamu. Mfereji huo ulikuwa mtangulizi wa Mfereji wa Suez unaofupisha safari za meli kati ya Ulaya na Asia.

Mifereji kati ya Bahari

hariri

Kati ya mifereji muhimu ya kimataifa kuna Mfereji wa Panama unaoruhusu kupita kati ya Atlantiki na Pasifiki pamoja na Mfereji wa Suez.

Kwa jumla mifereji ya maji ni sehemu muhimu za miundombinu wa kila nchi ama kama njia za kubeba mizigo kwa meli au kama njia ya kupeleka maji panapohitajika.

Mifereji barani

hariri

Mifereji ni muhimu pia ndani ya nchi nyingi. Kabla ya kupatikana kwa reli zilikuwa njia nyepesi na ya haraka kusafirisha mizigo kwa gharama nafuu.

 
Daraja la mfereji juu ya mto, Uingereza

Leo hii mahali pengi mifereji ya kihistoria imepitwa na wakati ilhali reli na usafiri wa barabarani hufikisha bidhaa haraka zaidi na kwa bei nafuu. Lakini mifereji ya kale siku hizi ni kuvutio cha utalii: inatumiwa na watu wanaopenda kusafiri kwenye maji.

Lakini mifereji inayoweza kubeba meli inaendelea kuwa na maana. Matumizi ya mifereji ya kimataifa yanazidi kuongezeka[2]. Hata ndani ya nchi usafiri kwa mifereji na mito mikubwa bado ni muhimu kwa bidhaa kama mchanga, mawe, kokoto, makaa na mafuta.

Milango ya mfereji

hariri

Changamoto kwa mfereji mara nyingi ni milima na mabonde kwenye njia yake. Wajenzi walijifunza tangu siku za Mfereji Mkuu wa China kuvuka mitelemko kwa kutumia milango ya mfereji. Hapa wanapanga sehemu ambako wanafunga njia ya maji kwa geti linalofuatwa na nafasi na geti la pili na hivyo kupata chemba baina ya milango miwili. Boti linaingia katika geti moja linalofungwa tena. Sasa maji yanaingizwa kwenye chemba na maji ndani yake yanapaa pamoja na boti. Mara maji ndani ya chemba yamepaa sawa na sehemu ya juu ya mfereji, mlango wa pili unafunguliwa na boti linaendelea. Kwa njia ya chemba mfululizo boti linaweza kushuka au kuinuliwa; meli kubwa zinazopita Mfereji wa Panama zinapanda na kushuka mita 26; meli hadi tani 5,000 kwenye mfereji baina ya mto Volga na Bahari Baltiki nchini Urusi hupanda mita 80 kwa njia ya milango.

Tanbihi

hariri
  1. Donald Langmead (2001). Encyclopedia of Architectural and Engineering Feats. ABC-CLIO. p. 37. ISBN 978-1-57607-112-0. Iliangaliwa Februari 2021. "the world's largest artificial waterway and oldest canal still in existence"
  2. Zamorano, Juan; Martinez, Kathia (June 26, 2016). "[https://web.archive.org/web/20160626050451/http://bigstory.ap.org/article/b8495e0dad974d39bf4147f647d2f831/panama-canal-opens-5b-locks-bullish-despite-shipping-woes Panama Canal opens $5B locks, bullish despite shipping woes]". The Big Story. Associated Press. Archived from the original on June 26, 2016. iliangaliwa 9 Machi 2021.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: