Lisbon
(Elekezwa kutoka Mkoa wa Lisbon)
Lisbona (kwa Kireno: Lisboa) ni mji mkuu wa Ureno, pia mji mkubwa wa nchi wenye wakazi 560,000; pamoja na rundiko la mji ni milioni mbili.
Lisbon | |||
| |||
Majiranukta: 38°42′00″N 09°08′00″E / 38.70000°N 9.13333°E | |||
Nchi | Ureno | ||
---|---|---|---|
Mkoa | Mkoa wa Lisbon | ||
Idadi ya wakazi | |||
- Wakazi kwa ujumla | 564,477 | ||
Tovuti: http://www.cm-lisboa.pt/ |
Mji uko kando ya mto Tejo kwenye kona ya kusini-magharibi ya Ulaya mwambaoni kwa Atlantiki.
Historia
haririMji ulijulikana tangu karne ya 3 KK kwa jina la "Olispo". Wakati wa Dola la Roma ulikuwa mji mkuu wa jimbo la Lusitania.
- 719 ulitwaliwa na Waarabu.
- 1147 Lisbon ilitwaliwa na mfalme Mreno Dom Afonso Henriques.
- 1256 mfalme Afonso III alihamisha mji mkuu kutoka Coimbra kuja Lisbon.
- 1499 Vasco da Gama alirudi Lisbon kutoka safari yake ya kwanza ya Uhindi akaanzisha kipindi cha utajiri kwa Ureno na mji kutokana biashara ya kikoloni.
- Karne ya 16: Lisbon imekua na kuwa mji mkubwa duniani unaojulikana wakati ule wenye wakazi 350,000.
- 1 Novemba 1755 tetemeko la ardhi liliharibu theluthi mbili za mji na kuua watu 60,000.
- 5 Oktoba 1910 Jamhuri ya Ureno ilitangazwa Lisbon.
- 1926: mapinduzi ya kijeshi yalimaliza demokrasia na kuanzisha kipindi cha udikteta katika Ureno
- 1974: mapinduzi ya kijeshi yalimaliza udikteta na kuanzisha kipindi kipya cha demokrasia
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Tovuti rasmi ya Lisbon
- Alfama & Castelo Ilihifadhiwa 13 Mei 2007 kwenye Wayback Machine.
- Picha za Lisbon
- Picha za Lisbon Ilihifadhiwa 19 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ureno bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lisbon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |