Kamerun (mlima)

(Elekezwa kutoka Mlima Kamerun)

Kamerun ni volkeno hai na mlima mkubwa nchini Kamerun wenye kimo cha m 4095 juu ya UB. Majina mengine ni Fako (jina la kilele cha juu) au Mongo ma Ndemi ("Mlima Mkubwa").

Kasoko za Mlima Kamerun
Kasoko za Mlima Kamerun

Mlima uko karibu na Ghuba ya Guinea ya Atlantiki na mji wa bandari Douala.

Milipuko imeripotiwa katika miaka 1650, 1807, 1825, 1838, 1852, 1865, 1866, 1871, 1909, 1922, 1925, 1954, 1959, 1982 na 1999 BK.

Kuna uwezekano ya kwamba tayari baharia Hanno wa Karthago alimaanisha mlima wa Kamerun alipoeleza habari za mlima wa "Gari la Miungu" uliotema moto kwa mwisho wa safari yake ya Afrika ya Magharibi mnamo mwaka 570 KK.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kamerun (mlima) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.