Mfereji wa Msumbiji

(Elekezwa kutoka Mozambique Channel)

Mfereji wa Msumbiji (kwa Kiingereza Mozambique Channel, kwa Kifaransa Canal du Mozambique, kwa Kimalagasi: Lakandranon'i Mozambika, kwa Kireno: Canal de Moçambique) ni sehemu ya Bahari Hindi iliyopo kati ya kisiwa cha Madagaska na bara la Afrika, hasa nchi ya Msumbiji.

Mahali pa Mfereji wa Msumbiji

Sehemu yake nyembamba yenye upana wa kilomita 460 iko kati ya Angoche, Msumbiji na Tambohorano, Madagaska. Urefu wake ni takribani km 1,600. Maji yake yanafikia kina cha mita 3,292 .

Mfereji huu unapitiwa na mkondo wa bahari unaopeleka maji ya vuguvugu hadi pwani ya Afrika Kusini.

Visiwa katika Mfereji wa Msumbiji hariri

Komori hariri

Maeneo ya ng’ambo la Ufaransa hariri

Iles Eparses (Visiwa vilivyotawanyika) hariri

Madagaska hariri

Msumbiji hariri

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons


18°S 41°E / 18°S 41°E / -18; 41