Ruaha Mkuu
Ruaha Mkuu (pia: Ruaha Mkubwa) ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto la Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake, si mbali na Iringa Mjini.
Chanzo na mwendo wa mto
haririChanzo chake ni mito mingi midogo inayotelemka milima ya nyanda za juu za kusini mwa Tanzania, hasa safu za milima ya Uporoto na ya Kipengere. Mito hii inakusanya maji yake kwenye tambarare ya Usangu na ndipo Ruaha inapoanza. Mito mikubwa zaidi inayoungana hapa na kuunda Ruaha ni pamoja na mto Mbarali, mto Kimani na mto Chimala.
Karibu na Ng’iriama mto unatoka katika Usangu na kuingia hifadhi ya kitaifa ya Ruaha. Inaendelea kupokea Ruaha Mdogo na mto Kisigo kabla ya kuingia katika ziwa la lambo la Mtera, halafu inaendelea hadi lambo la Kidatu.
Baada ya Kidatu, Ruaha Mkuu unapita tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji.
Matatizo ya ekolojia ya mto
haririMaji ya Ruaha Mkuu ni muhimu kwa ekolojia ya beseni lake pamoja na watu wote wanaoishi huko. Lakini matumizi ya binadamu yameleta mvurugo kwa ekolojia ya mto na tangu mwaka 1993 mto umeanza kukauka wakati wa ukame. Uhaba wa maji umesababishwa na matumizi mabaya ya maji upande wa miradi mikubwa ya mpunga katika Usangu.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Geonames.org
- WWF.org - The Ruaha Water Programme Ilihifadhiwa 15 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- Ruaha information with images Ilihifadhiwa 9 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
- FAO review
- FAO - fact sheet on the ecohydrology of the Great Ruaha River (2003) Ilihifadhiwa 11 Juni 2007 kwenye Wayback Machine.
- Öhman, May-Britt, Taming Exotic Beauties: Swedish Hydro Power Constructions in Tanzania in the Era of Development Assistance, 1960s - 1990s, Stockholm, 2007, PhD Thesis
7°56′S 37°52′E / 7.933°S 37.867°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ruaha Mkuu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |