Mtumiaji:Kipala/Archive 14

Kuhusu Wikipedia kwa simu hariri

Watu wengi wako Afrika wanasoma wikipedia kwa simu. Wanaweza kuhusu kwa simu pia?

https://www.mediawiki.org/wiki/Wikimedia_Apps

https://translatewiki.net/wiki/Translating:WikimediaMobile

Benson Muite (majadiliano) 12:35, 28 Januari 2020 (UTC)

Asante kwa swali, Ndugu Benson. Tuna watumiaji wengi wanaochangia kwa simu. Inawezekana, pia kwa matokeo mazuri. Historia ya makala inaionyesha kwa "tag:Mobile edit". Kwa upande mwingine tuna tatizo hasa kwa watumiaji wapya wakiamua mara moja kubadilisha kitu kidogo au kuongeza hosa, sentensi au neno kwamba hariri zao zina makosa (au:hazina maana) kwa hiyo tunasafisha mara kwa mara. Si rahisi kuunda makala marefu kidogo kwa simu ya mkononi. Lakini uwezekano upo. Kipala (majadiliano) 12:55, 28 Januari 2020 (UTC)
Kutafsiri kwa kutumia msaada kama translatewiki inawezakana pia, mimi mwenyewe ninaitumia siku hizi mara kwa mara. Hata hivyo, watumiaji wapya wanaonywa dhidi yake. Maana inahitaji maarifa na umakini. Ni rahisi kuingiza makala marefu ya Kiingereza katika programu ya aina hii, kusahihisha kidogo makosa ya kwanza na kuihifadhi. Ila tu mara nyingi (hasa kwenye skrini ndogo ya simu) watumiaji wanachoka au hawaoni tena makosa mengine - yanayobaki. Ni kidogo kama samaki hizi zenye sumu zinazopendwa na Wajapani - tamu sana, lakini ole ukisahau kukata sehemu za sumu! Kipala (majadiliano) 13:04, 28 Januari 2020 (UTC)

Kazi nzuri ya uhariri hariri

Habari!

Umefanya vyema kuweka kielelezo kwenda Mapatano ya Kimataifa dhidi ya Utesaji.

BlessNathan (majadiliano) 13:56, 1 Februari 2020 (UTC)

Kuhusu kubadili jina la mtumiaji hariri

Mimi Simon waziri msika naomba kubadili jina la mtumiaji na liwe 20_savage.Asante amani kwako--Simon waziri msika (majadiliano) 12:23, 7 Februari 2020 (UTC)kipala.

Mashindano ya Uhariri Alfagems hariri

Ndugu, nipo na Magotech kwa ajili ya mashindano yetu. Afadhali usihariri makala zinazoundwa mpaka tutoe tuzo kwa washindi. Asante. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:28, 16 Februari 2020 (UTC)

Usiwe na wasiwasi, naona hiyo baada ya tukio.Kipala (majadiliano) 18:53, 16 Februari 2020 (UTC)

Ugatuzi Burundi hariri

Ndugu, naona nchi hiyo ndogo imegawiwa sehemu 16 (provinces) ambazo tungeziita wilaya, si mikoa. Hasa kwa sababu kuna ngazi ya juu zaidi ambayo inafaa iitwe mkoa. Unasemaje? Kuhusu masahihisho yangu, nimekuelewa. Nitasubiri zaidi. Hofu yangu ni kusahau baadaye... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:43, 17 Machi 2020 (UTC)

Asante, kama wenzetu wa enwiki wako sawa https://en.wikipedia.org/wiki/Burundi#Subdivisions, zile provinces za Burundi ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi wa nchi. Je umeona ngazi ya juu? Menginevyo fanya unavyoona. Nadhani tu ni busara tukianza kutaja kwa kila nchi makala yetu husika, ambayo ni Eneo la utawala; tafadhali uiangalie, unatumia neno hili zuri "ugatuzi", labda uhamishe lemma kwenda kule. Sasa naona tuktaja mfano "wilaya/mikoa ya Burundi", tuwe na makala fupi inayosema "Wilaya/mikoa ya Burundi" inayoeleza kwa sentensi moja "Wilaya/Mikoa ya Burundi ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi wa nchi. Nchi hiyo imegwanywa kwa wilaya/mikoa 17. Wil/Mkoa unagawanywa kwa ....." Kipala (majadiliano) 06:23, 17 Machi 2020 (UTC)

Tafsiri hariri

Habari! naomba msaada wa tafsriri ya maneno haya : Performance of biofilm carriers in anaerobic digestion of sisal leaf waste leachate Czeus25 Masele (majadiliano) 15:41, 2 Aprili 2020 (UTC)

Kwa nini unataka kuitafsiri? ni jina la makala kuhusu utafiti fulani, haihitaji tafsiri. Ukitaka kuieleza usitafsiri utumie maneno yako. Kipala (majadiliano) 16:25, 2 Aprili 2020 (UTC)
Labda kitu kama "ufanisi wa (kipagazi ?) cha ukoga hai katika mmeng'enyo anerobi wa kichujuaji cha mikonge" - siridhiki kipagazi (carrier).Kipala (majadiliano) 18:13, 2 Aprili 2020 (UTC)

Masanja hariri

Nmeondoa picha ya Masanja kwa sababu ya mlalamikaji mmoja akisema anaomba kuondolewa kwa picha hiyo. Natafuta picha nyingine. Czeus25 Masele (majadiliano) 03:15, 11 Aprili 2020 (UTC)

Sawa si picha ya kupendeza sana. Basi kumbuka kufuta faili ya picha yenyewe, maana bado iko. Kipala (majadiliano) 05:57, 11 Aprili 2020 (UTC)
Naomba maelekezo namna ya kufuta picha. Czeus25 Masele (majadiliano) 06:51, 11 Aprili 2020 (UTC)
Unafungua picha, utaipata kwa kuingia katika historia ya makala. Katika historia fungua nakala yenye picha, bofya picha, utapata ukurasa wa faili yake. Hapa ukihariri unaweza kufuta nisipokosei. Kipala (majadiliano) 08:28, 11 Aprili 2020 (UTC)
Ahsante. Czeus25 Masele (majadiliano) 14:06, 11 Aprili 2020 (UTC)

Naomba msaada wa kusaidiwa kuhariri makala niliyoanzisha ya Yericko Nyerere.

Naomba kusaidiwa kuweka picha yake.

Naomba kusaidiwa kuweka mpangilio mzuri kulingana na sheria za Wikipedia ya kiswahili.

Mimi ni mgeni sina uzoefu wa kutumia Wikipedia lakini nimeona nianzishe ukurasa wa Yericko ambae ni mwandishi maarufu wa vitabu Afrika Mashariki na Mchambuzi wa Ulinzi na Usalama. Mbutublock (majadiliano) 03:58, 9 Septemba 2021 (UTC)

Programmu ya kusafishia sw.wikipedia hariri

Kuna programmu , nafikiri inaweza kusaida na Wikipedia ya Kiswahili. Programmu ingine ni . Au tunaweza kuandika yetu. Benson Muite (majadiliano) 12:34, 29 Aprili 2020 (UTC)

Translation request hariri

Hello.

Can you translate and upload the articles en:Azerbaijan SSR and en:Democratic Republic of Azerbaijan in Swahili Wikipedia? They certainly don't need to be long like the English versions.

Yours sincerely, Karalainza (majadiliano) 11:28, 13 Julai 2020 (UTC)

Kamusi na viongozi wa Wikipedia ya Kiswahili hariri

Ndugu, nimeona umefuta sehemu ya mchango wa mwalimu wetu Mengistu kwamba una mashaka nao. Naomba maelezo kidogo. Pia nimeona umeandika idadi ya viongozi wa mradi wetu si halisi kwa sababu miaka ya nyuma tulisita kuondoa wale waliopumzika muda mrefu. Je, hatuwezi sasa kuchukua hatua? Amani kwako!--Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:29, 22 Julai 2020 (UTC)

Kuhusu "Kamusi" nimeona hasa muhimu kuhamisha sehemu kuhusu "Historia" nyuma, maana iliwekwa kabla ya maelezo ya kimsingi kuhusu aina tofauti za kamusi. Inawezekana katika kukata na kubandika tena nilifuta zaidi kuliko jinsi nilivyokusudia. Nitaangalia tena. Sehemu ya historia inajaa makosa mengi, hasa sehemu kuhusu kamusi za Kiswahili. Majina yameharibika mno (Sowahili si jina, wala Smee wala Salt walitunga kamusi, walikusanya maneno kadhaa tu kama mifano ya lugha; "Esteere" ni askofu Edward Steere, "Krafp (1845)" ni Ludwig Krapf. -- Kifungu chote kuhusu Kigiriki kimenakiliwa kutoka makala Kigiriki lakini hakina uhusiano na mada ya Kamusi. Niliandika "mashaka" kwa sababu sijakuwa na muda wa masahihisho.
Kuhusu wakabidhi: sawa, twende! Miaka iliyopita ni hasa Oliver ambaye hakupenda kufuta. Mimi mwenyewe naona kama mtu hakuonekana mwaka mmoja afutwe katika hadhi ya mkabidhi. Wikipedia nyingine zinaangalia pia kama mkabishi anatekeleza shughuli zake au la. Kipala (majadiliano) 08:49, 23 Julai 2020 (UTC)
Hata mimi naona hivyo: kimya cha mwaka mmoja kiwe kigezo. Tunawashukuru waliofanya kazi, lakini kuwaacha kama majina tu hakuna uhalisia... --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:37, 23 Julai 2020 (UTC)

Foto hariri

Hallo Kipala,
Das Foto, das im Artikel zur SGR steht, ist eine Urheberrechtsverletzung und wird demnächst gelöscht. Um zu vermeiden, dass in dem Artikel ein kaputter Bildlink ist, habe ich es durch ein anderes Foto bereits im Vorhinein ersetzt. Würdest du deine Änderung also wieder zurücksetzen – oder alternativ ein anderes Foto nehmen? Viele Grüße, --Jcornelius (majadiliano) 22:59, 3 Agosti 2020 (UTC)

Dein Foto ist noch drin im Artikel. Kipala (majadiliano) 16:06, 4 Agosti 2020 (UTC)
Ich verstehe nicht. Auf welchen Artikel wird verwiesen? Ich sehe kein neues Foto in Nzige-jangwa (SGR). ChriKo (majadiliano) 14:40, 5 Agosti 2020 (UTC)
Inahusu Reli_ya_SGR_ya_KenyaKipala (majadiliano) 17:35, 6 Agosti 2020 (UTC)

Mitaa hariri

Ndugu, naomba uangalie maswali yangu ya leo katima majadiliano ya kurasa mbalimbali. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:15, 17 Agosti 2020 (UTC)

Naona swali lako leo tu. Siwezi kuona tena mabadiliko ya jana. Unamaanisha makala zipi?Kipala (majadiliano) 07:22, 17 Agosti 2020 (UTC)
Ndiyo, leo, si jana! Ni Rutamba, Malunde na Madume bora. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:59, 17 Agosti 2020 (UTC)

Naomba kuzirudisha upya na kutoa uthibitisho Silent ocean Tanzania,Counsellorsalah hariri

Kipala Nimeona sababu iliyotolewa kwa ajili ya ufutaji wa makala hizo mbili, nimejifunza jambo juu ya uundaji wa makala hapa wiki. kama ulivyoelezea kwenye ukurasa wa makala ya ufutaji, nilijaribu kuziingiza enwiki lakini zilikosa mantiki. nipo katika kujifunza kuhariri hapa wiki ili na mimi baadae niweze kuisaidia swwiki katika makala tofauti tofauti. hivyo naomba kuanzisha tena makala hizo mbili ambazo tayari zimefutwa, na kwa sababu ambazo ni sahihi, ila nimefanyia marekebisho sababu ya awali na kufupisha maneno, na kuelezea kile tu ambacho kina uthibitisho. ahsante. molee4real (majadiliano)

Lambo la Kihansi hariri

habari Kipala, naomba msaada namna ya kutumia google maps kwenye ukurasa wangu wenye jina tajwa. Asante --Olimasy (majadiliano) 12:44, 18 Septemba 2020 (UTC)

Pia angalia namna ya kutumia "l" na "r". --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:29, 18 Septemba 2020 (UTC)
Mimi mwenyewe sijaelewa bado namna ya kutumia google map pamoja na misimbo ya majiranukta. ninabahatika wakati mwingine kama tunayo infobox iliyoandaliwa kuwa na majiranukta. Ninafikiri tatizo ni hii: tuna infoboxes kadhaa ambazo ni za zamani kabla ya kusanifishwa kwa infoboxes kwenye enwiki jinsi iivyo. Kama tungempata mtu anayeangalia boxes zetu na zile za kawaida za kimataifa tunagweza kuzitafsiri na kutumia. Nahisi hapa tupange warsha ya pekee kwa njia ya zoom, kwa kuomba msaada wa wale wanaojua nje ya swwiki. Mimi hutumia mbinu wangu: nafungua openstreetmap (shauri ya laiseni ya hakimiliki), nachukua pcha ya skrini, naipeleka programu kama PAINT, naweke alama ya mahali pamoja na matini ya Kiswahili, naipakua kwenda commons, basi nimeunda picha ya ramani ninayotumia. Kipala (majadiliano) 19:05, 18 Septemba 2020 (UTC)

We sent you an e-mail hariri

Hello Kipala/Archive 14,

Really sorry for the inconvenience. This is a gentle note to request that you check your email. We sent you a message titled "The Community Insights survey is coming!". If you have questions, email surveys@wikimedia.org.

You can see my explanation here.

MediaWiki message delivery (majadiliano) 18:54, 25 Septemba 2020 (UTC)

Idadi ya makala hariri

Ndugu, imekuwaje tangu siku chache idadi ya makala za Kiswahili imekatwa kama 800: toka 60,300 hivi zimebaki 59,500 tu? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:18, 27 Septemba 2020 (UTC)

Swali zuri, nimeiona pia, sijui. Najaribu kuuliza. Kipala (majadiliano) 11:43, 27 Septemba 2020 (UTC)
Pia nimeona haririo lako la mwisho kuhusu wasomaji wetu: kutoka milioni 4 wamekuwa chini ya 2. Idadi ya mwisho inalingana na ile ya wasomaji kwa nchi, lakini ile ya kwanza ipo katika Wikistat: ina maana gani? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:38, 28 Septemba 2020 (UTC)
Niliangalia wikistats na kuona namba za milioni 4. Baadaye niliangalia toolforge ambako ni chini ya mio 2. Nimekumbuka nimewahi kuona hii lkn nilishau. Basi ukifungua https://stats.wikimedia.org/#/sw.wikipedia.org/reading/total-page-views/normal%7Cbar%7C2-year%7C~total%7Cmonthly unaona idadi ya kuangaliwa kwa swwiki. Ukibofya "Split by agent type" (ambacho nilisahau) unaona kiasi gani cha watu halisi na kiasi gani cha bots au programu za crawler. Namba ya watu halisi ni sawa na namba inayoonyeshwa pale toolforge https://pageviews.toolforge.org/siteviews/?platform=all-access&source=pageviews&agent=user&start=2019-09&end=2020-08&sites=sw.wikipedia.org. Kipala (majadiliano) 08:44, 28 Septemba 2020 (UTC)

Swahili Wiktionary hariri

Saalam, maneno ambayo yapo kwenye sw wiktionary yana hitilafu kidogo. Maneno ambayo hayafahi kuwepo au katika lugha zingine vinaongezeka, sina uwezo wa kuzitoa kwenye wiktionary tafadhali zitoe, au unipe usaidizi wa jinsi nawezaya kuyatoa maneno hayo.Alvin kipchumba (majadiliano) 12:15, 30 Septemba 2020 (UTC)

Naona umeanzisha mwenyewe makala ya "kuadhiminisha" ambayo si Kiswahili. Kwa nini? Mimi sina mamlaka pale Wikamusi, ongea na wakabidhi wa pale, unawakuta kwenye ukurasa wa Jumuia. Kipala (majadiliano) 15:04, 30 Septemba 2020 (UTC)
(en) If i can weigh in here, the Swahili Wiktionary is really in a mess and i have been going on trying to fix things. If you can help out in any way with the kamusi or otherwise invite users who might be intrested it would be appreciated. Cheers --Synoman Barris (majadiliano) 11:57, 2 Oktoba 2020 (UTC)
(en) I was there some days ago. Couldn't do much more since I have a limit access to the site. Though I can fix some error if pointed where!--'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 13:27, 2 Oktoba 2020 (UTC)

Kanisa la Mwenyezi Mungu hariri

I figured, that I could spread the word about The Church of Almighty God (or "Kanisa la Mwenyezi Mungu" as it's officially called in Swahili), which is also known as Eastern Lightning (or Umeme wa Mashariki).

Here are some links to be shared:

Do you mind if I make a personal userpage for an English mock-up of a Swahili article on The Church of Almighty God?

Thanks for reading. --Apisite (majadiliano) 05:26, 2 Novemba 2020 (UTC)

Mpendwa, unachofanya kwenye ukurasa wako wa mtumiaji ni shauri lako, usipoleta matangazo ya kibiashara au haramu au matusi. Ila matini za Kiingereza hazidumu hapa kwenye makala, tunafuta. Pia kama unaweza kutunga makala inayoleta habari halisi, sawa ni kama kila mada. Sieelwei uanchomaanisha ukisema "spread the word"- Kipala (majadiliano) 20:57, 2 Novemba 2020 (UTC)

Kundi la whatsapp la wakabidhi hariri

Habari Kipala! Nilipata ujumbe wako. Kundi la whatsapp la wakabidhi ni wazo zuri. Nimepotea whatsapp wiki iliyopita kutokana na changamoto binafsi, natarajia kurejea wiki hii. Nitakutaarifu. Asante. Mtumiaji:Aneth David (SLU) Majadiliano ya mtumiaji:Aneth David (SLU)

Nimeona majadiliano yenu. Jumapili iliyopita watu mbalimbali walichangia Wikipedia yetu kwa tafsiri za kompyuta. Labda tufikie uamuzi wa moja kwa moja za kuzifuta au kutafsiri upya sehemu ndogo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:47, 18 Desemba 2020 (UTC) S