Nino wa Georgia (kwa Kigeorgia: წმინდა ნინო, ts'minda nino, kwa Kigiriki Αγία Νίνα, Agia Nina) alikuwa mwanamke (296 hivi – 338 au 340) aliyeingiza Ukristo nchini Georgia, na kwa sababu hiyo anaitwa "Aliye sawa na Mitume" na "Mwangazaji wa Georgia".

Picha takatifu ya Mt. Nino wa Georgia.
Mt. Nino.
Mt. Nino na gombo lake na msalaba wa mzabibu.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake kwa kawaida huadhimishwa tarehe 14 Januari[1].

Maisha hariri

Kadiri ya mapokeo alitokana na familia ya Kirumi yenye kuongea Kigiriki kutoka Kolastra, Kapadokia na alikuwa na undugu na Joji mfiadini,[2]. Kutoka Konstantinopoli alikwenda Iberia kwenye milima ya Kaukasi kama mfungwa.

Vyanzo vingine vinasema alitokea Roma, Yerusalemu au Galia (leo Ufaransa). [3]

Kwa utakatifu wa maisha yake alijivutia heshima ya wote na kisha kutenda miujiza ya uponyaji, alimfanya malkia Nana wa Iberia aongokee Ukristo.

Halafu mfalme Mirian III wa Iberia alirudishiwa uwezo wa kuona baada tu ya kumuomba "Mungu wa Nino", akaongoka pia na kufanya Ukristo kuwa dini rasmi ya nchi hiyo (327 hivi).

Nino aliendelea na umisionari nchini hadi kifo chake.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. "Orthodox Church of America -". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-20. Iliwekwa mnamo 2014-09-30. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-01-01. Iliwekwa mnamo 2014-09-30. 

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.