Open main menu
Mahali pa Novaya Zemlya duniani, pamoja na mahali pa mlipuko wa bomu ya nyuklia
Ramani ya Novaya Zemlya (kiingereza)

Novaya Zemlya (rus. Но́вая Земля́ nchi mpya) ni funguvisiwa ya Urusi iliyopo kwenye Bahari Aktiki. Eneo lake ni kilomita za mraba 90,650. Kiutawala ni Wilaya ya Novaya Zemlya katika mkoa wa Arkhangelsk Oblast. [1]. Mwaka 2010 ilikuwa na wakazi 2,429 na karibu 2,000 waliishi katika mji wa Belushya Guba penye makao makuu ya wilaya.

Wakazi asilia walikuwa wavindaji na wavuwi wa kabila la Wanenets waliohamishwa kutoka visiwa katika miaka ya 1950 [2]. Wakati ule walikuwa watu wasiozidi 300. [3]. Uhamisho huu ulisababishwa na mipango ya kutumia visiwa kwa shughuli za kijeshi na majaribio ya kulipusha mabomu ya nyuklia.

Novaya Zemlya kuna visiwa viwili vikubwa vinavyotengwa kwa mlangobahari mwembamba mwenye upana wa mita 600 hadi kilomita chache. Mlima mkubwa uko kwenye kisiwa cha kaskazini mwenye kimo cha mita 1,547.

Hadi leo Novaya Zemlya ni kituo cha kijeshi na wakazi wengi ni wanajeshi na familia zao. Umoja wa Kisovyeti ulitumia visiwa kwa milipuko ya majaribio ya mabomu ya nyuklia; tar. 30 Oktoba 1961 mlipuko mkubwa wa kinyuklia katika historia ulitekelezwa hapa. Nguvu ya bomu ilikadiriwa kuwa na megatoni 50.

MazingiraEdit

Kijiolojia Novaya Zemlya ni endelevu la safu ya milima ya Ural.[4]. Uso wa nchi ni ya milima.[5]

Kisiwa cha kaskazini kuna barafuto nyingi, kisiwa cha kusini unafunikwa kwa tundra.[6]

Maliasili ni pamoja na shaba, plumbi na zinki.[6]


Viungo vya NjeEdit

MarejeoEdit

  1. Sheria ya Urusi #65-5-OZ
  2. Microsoft Word - North Test Site _FINAL_.doc (PDF). Iliwekwa mnamo 2012-09-27.
  3. Microsoft Word - North Test Site _FINAL_.doc (PDF). Iliwekwa mnamo 2012-09-27.
  4. Novaya Zemlya, Northern Russia. NASA. Iliwekwa mnamo 2006-10-14.
  5. Novaya Zemlya in: Encyclopaedia Britannica (11th ed.) (1911). Iliwekwa mnamo 2006-10-14.
  6. 6.0 6.1 Novaya Zemlya in: The Columbia Encyclopedia, 6th ed.. Iliwekwa mnamo 2006-10-14.