Nyasi-bahari
Nyasi-bahari | ||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyasi-bahari majani-membamba (Halodule uninervis)
| ||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||
| ||||||||
Ngazi za chini | ||||||||
Familia 4 |
Nyasi-bahari ni mimea ya baharini ya familia 4 za oda Alismatales: Cymodoceaceae, Hydrocharitaceae, Posidoniaceae na Zosteraceae, inayofanana na nyasi za kweli (Poales: Poaceae).
Ekolojia
haririKama mimea yote ya autotrofiki, nyasi-bahari zinafanya usanidimwanga katika maeneo chini ya maji yanayopata nuru na hutokea zaidi katika maji ya kipwani yanayokingwa ambapo zimeangika kwenye sakafu za mchanga au matope. Takriban spishi zote zinapitia uchavuchaji chini ya maji ya bahari na kukamilisha mzunguko wa maisha yao chini ya maji.
Nyanja za nyasi-bahari zinaweza kuwa ama monospesifiki (yenye spishi moja) au zenye spishi zilizochanganywa. Katika maeneo ya wastani, kwa kawaida spishi moja au chache hutawala (kama vile nyasi-bahari majani-mikunga Zostera marina katika Atlantiki ya Kaskazini), lakini nyanja za kitropiki kwa kawaida ni anuwai zaidi, spishi 13 zikiwa zimeandikwa nchini Ufilipino.
Nyanja za nyasi-bahari ni mifumekolojia anuwai yenye kuzalisha, na zinaweza kuhifadhi mamia ya spishi zinazohusishwa kutoka kwa faila zote, kwa mfano samaki wachanga na wapevu, miani na viani ya kiepifiti na inayoishi huria, moluska, daa-manyoya na minyoo-kuru. Spishi chache zilizingatiwa awali kujilisha moja kwa moja kwenye majani ya nyasi-bahari (kwa sababu moja maudhui yao ya chini ya lishe), lakini ukaguzi wa sayansi na mbinu bora za kufanya kazi zimeonyesha kuwa kula kwa nyasi-bahari ni kiungo muhimu katika mfuatano wa ulishano, na kulisha mamia ya spishi zinazojumuisha kasa, nguva, samaki, mabata bukini, mabata-maji, chani na kaa. Spishi fulani za samaki ambazo zinatembelea au kujilisha kwa nyasi-bahari hulea wachanga wao kwenye kapa au miamba ya kupakana.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Cymodocea rotundata (Cymodocea rotundata)
- Cymodocea serrulata (Cymodocea serrulata)
- Enhalus acoroides, Nyasi-bahari Majani-mishipi (Strapleaf seagrass)
- Halodule uninervis, Nyasi-bahari Majani-membamba (Narrowleaf seeagrass)
- Halodule wrightii, Nyasi-bahari wa Kingo-mchanga (Shoal grass)
- Halophila minor (Halophila minor)
- Halophila ovalis, Nyasi-bahari Nguva (Dugong grass)
- Halophila stipulacea (Halophila stipulacea)
- Syringodium isoetifolium Nyasi-bahari Majani-micheche (Syringodium isoetifolium)
- Thalassia hemprichii, Nyasi-bahari Kasa (Pacific turtle grass)
- Thalassodendron ciliatum, Nyasi-bahari Majani-miundu (Sickle-leaved cymodocea)
- Zostera capensis, Nyasi-bahari Majani-mikunga (Cape eelgrass)
Picha
hariri-
Nyasi-bahari majani-mishipi
-
Nyasi-bahari wa kingo-mchanga
-
Nyasi-bahari majani-micheche