Panjshir (kwa Kiajemi: پنجشیر) ni jina la mkoa mmojawapo wa Afghanistan, linalotokana na mto Panjshir unaopita katika mkoa huo. Bonde la Panjshir ni kitovu cha mkoa.

Mahali pa Panjshir nchini Afghanistan
Bonde la Panjshir

Jina "Panjshir" linamaanisha "Simba Tano" katika lugha ya Kiajemi.

Makao makuu yako kwenye mji wa Bazarak. Mkoa uko karibu km 100 kaskazini mashariki mwa Kabul, mji mkuu wa nchi.

Idadi ya wakazi ni kama 153,500 na eneo la mkoa ni kilomita za mraba 3,610. Lugha kuu katika mkoa huo ni Kidari, ambayo ni lahaja ya Kiajemi ya Afghanistan. Wakazi wengi ni Watajiki [1].

Wenyeji wa Panjshir wamekuwa maarufu kutokana na upinzani wao dhidi ya mamlaka ya nje.

Wakati wa uvamizi wa Umoja wa Kisovyeti katika Afghanistan, Jeshi Jekundu lilishambulia bonde la Panjshir mara nyingi lakini lilipaswa mara kwa mara kuondoka tena. Vivyo hivyo wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyofuata kuondoka kwa Warusi, Taliban walijaribu kuvamia Panjshir lakini walishindwa pia.

Baada ya ushindi wa pili wa Taliban kwenye Agosti 2021, Panjshir ilibaki kuwa mkoa wa mwisho ambao haudhibitiwi na Taliban nchini Afghanistan.[2]<ref>"Home". Northern Alliance: Fighting for a Free Afghanistan (kwa en-US). Friends of the Northern Alliance. Iliwekwa mnamo 20 August 2021.  Check date values in: |accessdate= (help)

Tanbihi hariri

  1. "Afghanistan". Library of Congress Country Studies. Library of Congress. 1997. Iliwekwa mnamo 2006-11-19. 
  2. "As Taliban takes over, one Afghan province is still standing strong – Here's the story of Ahmad Shah Massoud and his bastion Panjshir". Free Press Journal (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-17. 

Viungo vya Nje hariri

  • Bonde la Panjshir, gazeti la Nipashe 28.08.2021 (makala yenye makosa madogo ya kihistoria)
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: