Papa Boniface II alikuwa Papa kuanzia tarehe 20/22 Septemba 530 hadi kifo chake tarehe 17 Oktoba 532[1][2]. Alitokea Roma, Italia[3], lakini alikuwa Mwostrogoti, Papa wa kwanza mwenye asili ya Kigermanik[4].

Papa Bonifasi II.

Alimfuata Papa Felisi IV akafuatwa na Papa Yohane II.

Aliteuliwa na mtangulizi wake awawekwa wakfu na kuvishwa taji la kipapa tarehe 22 Septemba 530. Mpinzani wake, antipapa Dioscorus, aliyechaguliwa na wingi wa mapadri wa Roma, aliwekwa wakfu siku hiyohiyo lakini alifariki siku 22 baadaye.

Uamuzi muhimu zaidi aliouchukua ni kupitisha mafundisho ya Mtaguso wa Orange (529) kuhusu haja ya neema kwa wokovu[5].

Mazishi yake yalifanyika tarehe 17 Oktoba 532.

Tazama pia

hariri

Maandishi yake

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2.   Peterson, John Bertram (1913). "Pope Boniface II". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company.
  3. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  4. Paolo Bertolini, Bonifacio II, papa in https://www.treccani.it/enciclopedia/papa-bonifacio-ii_%28Dizionario-Biografico%29/
  5. "Pope Boniface II". Catholic Encyclopedia (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2017-03-17.

Marejeo

hariri
  • Sessa, Kristina (2012). The Formation of Papal Authority in Late Antique Italy: Roman Bishops and the Domestic Sphere. Cambridge University Press.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Boniface II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.