Papa Felix IV

(Elekezwa kutoka Papa Felisi IV)

Papa Felix IV (490 hivi - 20/22 Septemba 530) alikuwa Papa kuanzia tarehe 12 Julai 526 hadi kifo chake[1]. Alitokea Campania, Italia[2]. Baba yake aliitwa Castorius.

Mozaiki ya Mt. Felisi IV.

Alimfuata Papa Yohane I akafuatwa na Papa Bonifasi II.

Alichaguliwa kwa kumridhisha mfalme Theodoriko Mkuu akaweza kupata kwake fadhili mbalimbali kwa Kanisa Katoliki[3]. Mfalme alipofariki mwaka uleule, Felix aliweza kuendesha Kanisa kwa uhuru zaidi[4].

Aligeuza mahekalu mawili ya Kipagani ya mjini Roma kuwa basilika la Wat. Kosma na Damiani na alipigania sana imani sahihi[5].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 12 Oktoba[6].

Tazama pia

hariri

Maandishi yake

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Felix IV kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.