Papa Dionysius alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Julai 259 hadi kifo chake tarehe 26 Desemba 269[1].

Papa Dionysius.

Alimfuata Papa Sisto II akafuatwa na Papa Felisi I.

Alifanya kazi kubwa ya kupanga upya Kanisa baada ya dhuluma ya kaizari Valerian iliyoacha Roma bila askofu kwa karibu mwaka mzima[2]. Alitumia uhuru uliopatikana upya chini ya kaisari Gallienus na kudumu miaka 40[3].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Desemba[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. Kirsch, Johann Peter (1909). "Pope St. Dionysius" in The Catholic Encyclopedia. Vol. 5. New York: Robert Appleton Company.
  3. Eusebius, Historia Ecclesiastica, 7.13; translated by G.A. Williamson, Eusebius: The History of the Church (Harmonsworth: Penguin, 1965), p. 299
  4. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Maandishi yake

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Dionysius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.