Papa Klementi I
Papa Klementi I alikuwa Papa kuanzia takriban 92 hadi kifodini chake takriban 99[1]. Alitokea Roma, Italia.
Alimfuata Papa Anacletus akafuatwa na Papa Evaristus.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini na kutajwa katika Kanuni ya Kirumi.
Sikukuu yake ni tarehe 23 Novemba katika Ukristo wa magharibi[2] na tarehe 24 Novemba au 25 Novemba upande wa mashariki.
Maandishi
haririMaandishi pekee ambayo kwa hakika ni ya kwake ni waraka aliowaandikia Wakristo wa Korintho ili kuimarisha umoja na amani kati yao na kudhibiti uasi wao dhidi ya viongozi halali[3].
Kwa ajili hiyo Klementi anahesabiwa kuwa wa kwanza kati ya Mababu wa Kanisa waliofahamu Mitume wa Yesu[4]. Inawezekana ndiye aliyetajwa na Mtume Paulo katika Waraka kwa Wafilipi (4:3).
Sala yake
haririWewe umefunua macho ya mioyo yetu, ili tukujue wewe Mungu pekee, uliye juu sana katika mbingu za juu, mtakatifu unayekaa kati ya watakatifu, ambaye unanyenyekeza ufidhuli wao wenye kiburi, unabatilisha mashauri ya mataifa, unawainua juu wanyonge na kuwashusha wanaojikweza, wewe ambaye unatajirisha na kufukarisha, unaua na kuhuisha, ambaye peke yako unafadhili roho na ni Mungu pekee wa kila mwenye mwili, unatazama vilindi, unachunguza matendo ya wanadamu, unawasaidia waliopo hatarini na ni mkombozi wa waliokata tamaa, ni muumbaji na mtunzaji wa roho zote, unazidisha mataifa duniani, ambaye kati ya wote umewachagua wanaokupenda, kwa njia ya Yesu Kristo Mwanao mpendwa, ambaye kwa njia yake umetulea, umetutakasa na kutuvika heshima.
Tunakusihi, Bwana, uwe kwetu msaidizi na tegemeo. Uwakomboe walio taabuni kati yetu, uwahurumie wanyonge, uwainue walioanguka, ujidhihirishe kwa wahitaji, uwaponye wagonjwa, uwarudishe waliojitenga na taifa lako, uwashibishe wenye njaa, uwafungue wafungwa wetu, uwaimarishe walio dhaifu, uwatulize walio duni.
Mataifa yote wapate kujua ya kuwa ndiwe Mungu, wewe peke yako, na ya kuwa Yesu Kristo ni Mwanao nasi tu wako wako na kondoo wa malisho yako.
Tazama pia
hariri- Didakè yaani Mafundisho ya Mitume Kumi na Wawili na Waraka wa Mt. Klementi kwa Wakorinto, tafsiri ya B. Santopadre n.k. – ed. E.M.I. – Bologna (Italia) 1990 – ISBN 88-307-0321-4
Tanbihi
hariri- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
- ↑ "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Pope St. Clement I". www.newadvent.org. Iliwekwa mnamo 2022-01-21.
- ↑ http://www.santiebeati.it/dettaglio/30150
Vyanzo
hariri- Clement of Rome (1885b). The First Epistle of Clement to the Corinthians. IX. Wikisource.
- Durant, Will (2011). [[[:Kigezo:Google books]] The Story of Civilization]. Juz. la IV: The Age of Faith. Simon and Schuster. ISBN 978-1-4516-4761-7.
{{cite book}}
: Check|url=
value (help) - González, Manuel Hernández (2007). Fiestas y creencias en Canarias en la Edad Moderna. Ediciones IDEA. ISBN 978-84-8382-107-7.
- Kelly, John Norman Davidson; Walsh, Michael J. (2005). The Oxford Dictionary of Popes (tol. la 2nd). Oxford University Press. ISBN 978-0-19-861433-3.
- Libreria Editrice Vaticana (2008). Annuario pontificio (2008). Libreria Editrice Vaticana. ISBN 978-88-209-8021-4.
- Phan, Peter C. (2000). The Gift of the Church: A Textbook on Ecclesiology in Honor of Patrick Granfield, O.S.B. Liturgical Press. ISBN 978-0-8146-5931-1.
Marejeo mengine
hariri- Clarke, W. K. Lowther, mhr. (1937). The First Epistle of Clement to the Corinthians. London: Society for the Promotion of Christian Knowledge.
- Grant, Robert M., mhr. (1964). The Apostolic Fathers. New York: Nelson.
- Loomis, Louise Ropes (1916). The Book of Popes (Liber Pontificalis). Merchantville, NJ: Evolution Publishing. ISBN|1-889758-86-8.
- Lightfoot, J.B. (1890). The Apostolic Fathers. London: Macmillan.
- Meeks, Wayne A. (1993). The origins of Christian morality : the first two centuries. New Haven: Yale Univ. Press. ISBN 978-0-300-05640-2.
- Richardson, Cyril Charles (1943). Early Christian Fathers. The Library of Christian Classics. Philadelphia: Westminster Press.
- Staniforth, Maxwell (1968). Early Christian writings. Baltimore: Penguin.
Viungo vya nje
hariri- "Saint Clement I." Encyclopædia Britannica Online.
- "Pope St. Clement I". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
- Two Epistles Concerning Virginity .
- Opera Omnia
- Hieromartyr Clement the Pope of Rome Eastern Orthodox icon and synaxarion
- Patron Saints Index: Pope Saint Clement I
- Saint Clement at the Christian Iconography web site
- "Here Followeth the Life of St. Clement" in the Caxton translation of the Golden Legend
- "St. Clement of Rome, Pope and Martyr (1st Century)"
- Colonnade Statue in St Peter's Square