Papa Silvester I

Papa Silvesta I na Kaisari Konstantino Mkuu.

Papa Silvester I alikuwa papa kuanzia 31 Januari, 314 hadi kifo chake tarehe 31 Desemba, 335.

Alimfuata Papa Miltiades akafuatwa na Papa Marko.

Mtoto wa Rufinus, mkazi wa Roma, hatuna habari nyingi za maisha yake. Ila ni kwamba aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda mrefu mara baada ya Kaisari Konstantino Mkuu kulipatia uhuru wa dini na kulijengea maabadi mengi, makubwa na mazuri.

Wakati wake ulifanyika mtaguso mkuu wa kwanza (Nisea, leo nchini Uturuki, 325). Yeye hakuhudhuria, ila alituma wajumbe wawili akathibitisha maamuzi yaliyofikiwa.

Tazama piaEdit

Maandishi yakeEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Silvester I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.