Pat Thomas (mwanamuziki wa Ghana)

Pat Thomas (jina la kuzaliwa Nana Kwabena Amo Mensah [1]; alizaliwa Agosti 14, 1946) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Ghana. Anajulikana sana kwa kazi yake katika bendi za highlife za Ebo Taylor . [2]

Pat Thomas, mnamo Mei 2016 huko Ljubljana, Slovenia

Maisha ya awali na elimu hariri

Pat Thomas alizaliwa huko Ashanti nchini Ghana. Baba yake alikuwa mwalimu wa nadharia ya muziki na mama yake kiongozi wa bendi.

Kazi hariri

Alianza kazi yake ya muziki katika miaka ya 1960 ambapo alishirikiana na Ebo Taylor . [3] Mnamo 1974, aliunda bendi ya "Sweet Beans", alirekodi albamu yake ya kwanza ya False lover . Alirekodi albamu yake ya pili ya " Pat Thomas Introduces Marijata" akiwa na bendi ya Marijata. [4] Baada ya mapinduzi ya Ghana mwaka 1979, alihamia Berlin na baadae kuishi Kanada. Sasa anazunguka ulimwenguni kote na bendi yake ya Kwashibu Area. Mnamo Juni 2015 walitoa albamu ya Pat Thomas and Kwashibu Area Band [5] kuadhimisha miaka 50 ya kazi yake ya muziki. [6] Thomas anajulikana kama "The Golden Voice Of Africa".

Tuzo hariri

Mnamo mwaka 2015, albamu yake ya Pat Thomas and Kwashibu Area Band iliorodheshwa na AllMusic kama mojawapo ya "Albamu za Kilatini Zinazopendwa na Ulimwenguni". [7]

Marejeo hariri

  1. "First international release for Ghanaian legend Pat Thomas". Music In Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-05-26. 
  2. "Pat Thomas and Kwashibu Area Band". Music In Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-01-30. 
  3. "Patrick Thomas, Highlife Artist". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-03-22. Iliwekwa mnamo 2018-04-23. 
  4. "Pat Thomas homepage". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-20. Iliwekwa mnamo 10 Dec 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  5. "Pat Thomas & Kwashibu Area Band". Strut records. 12 Mar 2015. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-12-20. Iliwekwa mnamo 10 Dec 2016.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "Pat Thomas & Kwashibu Area Band". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 December 2016. Iliwekwa mnamo 10 Dec 2016.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  7. "Pat Thomas | Awards". AllMusic (kwa en-us). Iliwekwa mnamo 2020-01-30.