Peter Tabichi

Peter Tabichi ni mtawa wa Shirika la Wafransisko na mwalimu wa hisabati na fizikia katika shule ya sekondari ya Keriko katika kaunti ya Nakuru nchini Kenya.

Jina la kuzaliwa Peter Tabichi
Amezaliwa 1982, Nyamira County, KE
Kazi yake mwalimu wa sayansi

Ameshinda mwaka 2019 Tuzo ya Mwalimu Bora Ulimwenguni kutoka Shirika la Varkey (Varkey Foundation).

Maisha ya awaliEdit

Alizaliwa mwaka 1982 katika kijiji kidogo cha Kenya. Peter Tabichi alipokuwa na miaka kumi na moja mama yake alifariki. Halafu, alilelewa na baba yake tu[1].

Alihamasishwa kuwa mwalimu kwa sababu watu wengi wa familia yake walikuwa walimu: baba yake, na baadhi ya wajomba na binamu zake[2]. Alitaka kutumia elimu kuwasaidia wanafunzi na familia zao.

Alisoma shahada ya kwanza Chuo kikuu cha Egerton katika Nakuru, Kenya[3]. Tabichi ni mtawa wa kanisa Katoliki[4]. Anatumia masuala ya dini kufundisha vizuri. Kazi yake ya kufundisha alianza katika shule ya binafsi.

KaziEdit

Tabichi alifundisha hisabati, fisikia, na kemia katika Shule ya Sekondari ya Keriko, kijiji cha eneo la pwani, kutoka mwaka 2016. Hicho kijiji ni maskini, watu wengi hawana pesa na vyakula vya kutosha[5]. Kuna masuala mengi kama vile ujauzito wa vijana, kuacha shule mapema, uhaba wa vifaa vya elimu[6]. Asilimia tisini na tano ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Keriko wana umaskini. Tabichi amefanya kazi nyingi kuwasaidia wanafunzi wa kijiji. Tabichi hutumia asilimia themanini ya mshahara wake kuwalipia vitabu na sare wanafunzi wake[7].

Ameanza Klabu ya Kukuza Talanta na Klabu ya Imani shuleni[8]. Pia amechangia Klabu ya Sayansi. Wanafunzi wa Tabichi wamekamilisha vitu vingi. Baadhi ya wanafunzi wake wameshindana raundi ya mwisho ya Maonyesho Duniani ya Sayansi na Uhandisi ya Intel. Mmojawapo ameshinda tuzo ya Royal Society ya Kemia[9]. Tabichi aliposhinda Tuzo ya Mwalimu Bora Ulimwenguni, ameuambia umma kwamba anataka kutumia tuzo ya dola milioni moja kuwatumia wanafunzi wa Kijiji cha Pwani na shule yao.

MarejeoEdit

  1. Peter Tabichi: 10 things to know about Kenyan monk-teacher who won $1 million (en). gulfnews.com. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.
  2. Caroline Chebet. Peter Tabichi: World’s best teacher donates 80% of his salary to the poor. Standard Digital News. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-04-03. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.
  3. "Peter Tabichi", Wikipedia (in English), 2019-12-06, retrieved 2019-12-11 
  4. Peter Tabichi: 10 things to know about Kenyan monk-teacher who won $1 million (en). gulfnews.com. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.
  5. Press, The Associated (2019-03-24), "Kenyan Teacher Who Aids Poor Wins $1 Million Global Prize", The New York Times (in en-US), ISSN 0362-4331, retrieved 2019-12-11 
  6. Jenny Anderson. A Kenyan teacher just won the $1 million Global Teacher Prize (en). Quartz. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.
  7. Coughlan, Sean (2019-03-24), Kenyan science teacher wins global prize (in en-GB), retrieved 2019-12-11 
  8. Peter Dockrill. Kenyan Science Teacher Who Gives 80% of His Salary Away Just Won a $1M Global Prize (en-gb). ScienceAlert. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.
  9. Meet Peter Tabichi, winner of the Global Teacher Prize 2019 (fr). Varkey Foundation. Iliwekwa mnamo 2019-12-11.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter Tabichi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.