Raphael wa Brooklyn

Raphael wa Brooklyn (kwa Kiarabu: قديس رافائيل من بروكلين; jina la awali: رفائيل هواويني , Raphael Hawaweeny; Beirut, Lebanoni, 20 Novemba 1860[1]Brooklyn, New York City, Marekani, 27 Februari 1915) alikuwa askofu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi, wa kwanza kupewa hiyo daraja takatifu katika bara la Amerika Kaskazini.[2]

Picha halisi ya Mt. Rafaeli.
Archimandrite Raphael alipofikia Amerika.

Baada ya kusomea Damascus (Syria), Konstantinopoli (Uturuki) na Kiev (leo nchini Ukraine), mwaka 1895 alitumwa na Tsar Nikola II wa Russia kuhudumia waumini Waorthodoksi waliohamia Marekani.

Mwaka 1904 alipewa uaskofu kwa ajili ya dayosisi ya Brooklyn. Hadi kifo chake alianzisha parokia 29, monasteri moja na الكلمة (The Word), gazeti la Kiarabu[3] .

Alitangazwa na sinodi ya Kanisa la Kiorthodoksi la Amerika (Orthodox Church in America = OCA) kuwa mtakatifu mnamo Machi 2000.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake au Jumamosi ya kwanza ya Novemba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "A Centennial Celebration for Brooklyn’s Only Saint", New York Times, 5 November 2015. Retrieved on 6 November 2015. 
  2. "St. Raphael of Brooklyn + First Saturday in November - Antiochian Orthodox Christian Archdiocese". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-09. Iliwekwa mnamo Mei 5, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "The Word Magazine". antiochian.org. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.