Rungwe (wilaya)

(Elekezwa kutoka Rungwe)

Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania na ina Postikodi namba 53500.

Mahali pa Rungwe (kijani) katika mkoa wa Mbeya.
Daraja la Mungu ni kati ya maajabu asilia ya wilaya hii.

Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi.

Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.

Jina la wilaya limetokana na kituo cha misheni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban km 20 kutoka Tukuyu.

Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde".

Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 273,536 [2] baada ya mwaka 2013 kata 11 kutengwa na Rungwe na kuunda Wilaya ya Busokelo.

Barabara kuu kutoka Dar es Salaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya.

Rungwe inapokea mvua nyingi na iko kati ya maeneo yenye rutuba sana katika Tanzania.

Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai.

Tanbihi

hariri
  1. "Tanzania.go.tz census/districts/rungwe". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-06-23. Iliwekwa mnamo 2004-06-23.
  2. https://www.nbs.go.tz

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Rungwe - Mkoa wa Mbeya - Tanzania  

Bagamoyo | Bujela | Bulyaga | Ibighi | Ikuti | Ilima | Iponjola | Isongole | Itagata | Kawetele | Kinyala | Kisiba | Kisondela | Kiwira | Kyimo | Lufingo | Lupepo | Makandana | Malindo | Masebe | Masoko | Masukulu | Matwebe | Mpuguso | Msasani | Ndanto | Nkunga | Suma | Swaya


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rungwe (wilaya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.