Sally Nyolo (Alizaliwa 1965, Lekié huko Kamerun) Sally Nyolo aliondoka nyumbani kwao akiwa na umri wa miaka 13 na kwenda kuishi katika mji wa Paris, Ufaransa. Nyolo alianza kazi yake ya uimbaji mwaka 1982 akifanya kazi na wasanii wengi wa Ufaransa na barani Afrika kwa kutengeneza muziki wa redio na kwenye sinema.

Sally Nyolo

Mwaka wa 1993, Nyolo alijiunga na kundi la Ubelgiji la acappella, Zap Mama, katika ziara yao ya kuzunguka duniani Nyolo akiwa na Zap Mama alikuwa akirekodi albamu ya Sabsylma, na rekodi mbili za live huko Japan, na Montreux.

Mwaka 1996, Nyolo alirekodi albamu yake ya kwanza ya solo, iliyoitwa Tribu (Tribe), iliyochapishwa na the Luafrica Label. Albamu iliyotolewa na Radio France Internationale mwaka 1997, ilikuwa fanikio la dunia nzima, kwa kuuza nakala zaidi ya 300,000.[1]

Baadhi ya albamu zake nyingine kadhaa - Multicti (1998), Beti (2000), Zaione (2002) - Isiolo hatimaye alirudi nchini Kameruni, ambapo alianzisha studio, kwa nia ya kuchunguza na kuendeleza muziki wa eneo hilo. "Ninakusudia kuuza utamaduni wa Kikameruni nje ya nchi kwa kuanzisha jumuiya ya kimataifa ya muziki ambayo itaunganisha wanamuziki vijana wa Kikameruni na wasanii wengine duniani kote," alisema Nyolo. Juhudi hizi zilisababisha albamu ya Studio ya Kamerun, iliyochapishwa mwaka 2006 na World Music Network.[2]

Mwaka 2014, Nyolo alishirikiana na COPILOT Music pamoja na Sound katika jalada la "Maria Caipirnha (Samba da Bahia)"la Carlinhos Brown. Mpangilio huu uliwakilisha vyombo vya muziki na mitindo ya cameroon kwa ajili ya kampeni za kidigitali katika Kombe la Dunia la FIFA la 2014.[3]

Nyolo huimba kwa Kifaransa, Kiarabu, Kiingereza, Kihispania, na lugha yake ya asili. Katika muziki wake, yeye huchanganya mitindo na midundo, akitumia sauti za msitu kwa mdundo wa mjini. Jarida la Boston Herald lilisema, "Nyolo ameweza kuiwakilisha vyema na kuchanganya Afrika Magharibi na mji mkuu wa Paris.

Marejeo

hariri
  1. Biography of Sally Nyolo, African Success, 11 September 2011
  2. Opposing Viewpoints in Context. Web. 3 Nov. 2014
  3. Young, Bob. "Singer is making her future with languages of her past." Boston Herald, 21 August 1998
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sally Nyolo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.