Sikukuu za Bikira Maria
Sikukuu za Bikira Maria ni siku za kalenda ya liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Kikristo zilizopangwa katika mwaka wa Kanisa[1] kufanya ukumbusho wa matukio ya maisha yake na mengineyo ya historia ya Kanisa.
Sikukuu hizo zinatofautiana kadiri ya imani ya madhehebu husika[2].
Heshima za Liturujia ya Kiroma kwa Maria
haririKatika liturujia ya Roma, mbali ya kumtaja Mama Bikira Maria katika kila Misa wakati wa sala ya ekaristi, kuna maadhimisho kwa heshima yake. Hapa yamepangwa kulingana na kiwango cha heshima hiyo:
- 8 Desemba – Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili
- 1 Januari – Bikira Maria Mama wa Mungu
- 25 Machi – Bikira Maria Kupashwa Habari
- 15 Agosti – Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni
- 31 Mei – Ziara ya Bikira Maria
- 8 Septemba – Kuzaliwa kwa Bikira Maria
- Mei-Juni - Mama wa Kanisa
- Juni – Moyo Safi wa Maria
- 15 Septemba – Bikira Maria wa Mateso
- 22 Agosti – Bikira Maria Malkia
- 7 Oktoba – Bikira Maria wa Rozari
- 21 Novemba – Bikira Maria Kutolewa Hekaluni
- 11 Februari – Bikira Maria wa Lurdi
- 13 Mei – Bikira Maria wa Fatima
- 16 Julai – Bikira Maria wa Mlima Karmeli
- 5 Agosti – Kutabaruku Basilika kuu la Bikira Maria
- 12 Septemba – Jina takatifu la Maria
- 10 Desemba – Bikira Maria wa Loreto
- 12 Desemba – Bikira Maria wa Guadalupe
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya hiari ya Mama wa Mungu.
Tanbihi
hariri- ↑ Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria: mashariki zinatumika tenzi na nyimbo mbalimbali, k.mf. Akatistos inayomuita “daraja linalounganisha dunia na mbingu”, “ngazi aliyoiona Yakobo” “kina kisichochunguzika kwa macho ya malaika” (Mwa 28:12); magharibi anaheshimiwa kwa rozari.
- ↑ Wakristo wanaomheshimu Bikira Maria wanajieleza kwamba hawamuabudu hata kidogo, lakini wanamtolea heshima ya juu kuliko watakatifu wengine. Tofauti ni kwamba Mungu tu anastahili kuabudiwa (kwa Kigiriki, ‘latria’) watakatifu wanapewa heshima (‘dulia’) na Bikira Maria heshima zaidi (‘yuper-dulia’). Kanisa Katoliki linakiri neema zote za Mungu zinampitia Maria.