Maria kutolewa hekaluni

Bikira Maria Kutolewa Hekaluni ni kumbukumbu ya liturujia inayoadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 21 Novemba[1][2].

Mchoro wa ukutani huko Skopje, Macedonia.
Mchoro wa Titian (1534-1538, Gallerie dell'Accademia, Venice).

Msingi hariri

Adhimisho linatokana na habari ambayo haipatikani katika Agano Jipya, ila katika Injili ya Yakobo. Humo inasimuliwa kwamba wazazi wa Bikira Maria, Yohakimu na Ana, ambao hawakuwa na watoto, walipata ujumbe kutoka mbinguni kwamba watapata mtoto.

Kama shukrani ya kupata mtoto wa kike, akiwa bado mdogo walimleta katika Hekalu la Yerusalemu ili kumweka wakfu kwa Mungu[3].

Huko alibaki hadi alipotolewa kwa Yosefu.[3][4]

Asili hariri

Sikukuu ilianzishwa kuhusiana na kutabaruku Basilika jipya la Mtakatifu Maria, lililojengwa mwaka 543 na kaisari Justinian I karibu na mabaki ya Hekalu la Yerusalemu.[4]

Kutoka Ukristo wa mashariki sikukuu ilienea katika monasteri za Italia Kusini katika karne ya 9, ikaingia katika liturujia ya Papa wa Avignon mwaka 1372 kwa agizo la Papa Gregori XI.[5][6]

Picha hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. Some but not all Eastern Rite churches reckon by the Julian calendar, in which this date falls 13 days later on December 4 of the Gregorian calendar.
  3. 3.0 3.1 Peters, Sr. Danielle. "The Holy Land: In the Footsteps of Mary of Nazareth", Marian Library, University of Dayton. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-06-12. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
  4. 4.0 4.1 Mauriello, Matthew R., "November 21: Presentation of Mary", Fairfield County Catholic, 1996. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-10-03. Iliwekwa mnamo 2016-10-14.
  5. "The Saint Andrew Missal, with Sundays and Feasts," by Dom Gaspar LeFebvre, O.S.B., Saint Paul, MN: The E. M. Lohmann Co., 1952, p. 1684
  6. William E. Coleman, Ed. "Philippe de Mezieres' Campaign for the Feast of Mary's Presentation," Toronto: Pontifical Institute of Mediaeval Studies, 1981, pp. 3-4.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria kutolewa hekaluni kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.