Sipriani mfiadini
Sipriani (kwa Kilatini: Thascius Caecilius Cyprianus; 210 hivi - 14 Septemba 258) alikuwa askofu wa Karthago na mwandishi muhimu kati ya Mababu wa Kanisa, ambaye vitabu vyake vya Kilatini viko hadi leo [1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Septemba[2] pamoja na Papa Kornelio[3] kwa kuwa waliungana kushuhudia upendo kwa ukweli ule ambao haukubali kuyumbishwa na ambao wao waliuungama mbele ya Kanisa la Mungu na ulimwengu nyakati za dhuluma [4].
Maisha
haririAlizaliwa mwanzoni mwa karne ya 3 katika eneo la Afrika kaskazini, labda huko Karthago, alipopata elimu na kuwa mhubiri maarufu.
Baada ya kuongokea Ukristo kwa msaada wa padri Sesili (245), alipata mapema kuwa shemasi, padri akachaguliwa kuwa askofu mwaka 249 na hatimaye akafia dini.
Maandishi yake
haririYanapatikana katika magombo 3 na 4 ya Patrologia Latina.
Kitabu chake muhimu zaidi ni "De unitate ecclesiae" (Umoja wa Kanisa). Humo aliandika: "Hawezi kuwa na Mungu kama Baba yule asiye na Kanisa kama mama; . . . asiyekusanya katika Kanisa analitawanya Kanisa la Kristo" (vi.); "Hakuna nyumba nyingine kwa waamini isipokuwa Kanisa pekee" (ix.).
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Brent, Allen, editor and translator, "St Cyprian of Carthage: Selected Treatises," St. Vladimir's Seminary Press, 2007, ISBN 0-88141-312-7
- Brent, Allen, editor and translator, "St Cyprian of Carthage: Selected Letters," St. Vladimir's Seminary Press, 2007, ISBN 0-88141-313-5
- Daniel, Robin, "This Holy Seed: Faith, Hope and Love in the Early Churches of North Africa," (Chester, Tamarisk Publications, 2010: from www.opaltrust.org) ISBN 095385634
- Christian Classics Ethereal Library: Cyprian texts
- J.M. Tebes, "Cyprian of Carthage: Christianity and Social World in the 3rd. century", Cuadernos de Teología 19, (2000) (Kihispania)
Viungo vya nje
hariri- Cyprian and Roman Carthage Ilihifadhiwa 11 Novemba 2011 kwenye Wayback Machine. by Allen Brent(Cambridge, 2010).
- Pontius the Deacon (Pontius Diaconis), "The Life and Passion of Cyprian, Bishop and Martyr"
- "The Plague of AD 251" Archived 2012-12-20 at Archive.today
- Cyprian on the nature of the Church and Papacy by Dom John Chapman Ilihifadhiwa 9 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.
- Catholic Encyclopedia: St. Cyprian
- Works by Cyprian at the IntraText Digital Library, with concordance and frequency lists
- Acta proconsularia S. Cypriani
- Multilanguage Opera Omnia
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |