Chuma cha pua

(Elekezwa kutoka Steel)

Chuma cha pua (pia: chumapua, feleji) ni aloi wa chuma pamoja na gredi mbalimbali za kaboni ambayo imekuwa uti wa mgongo wa mapinduzi ya viwandani. Hadi leo ni msingi wa mashine na vifaa vingi, pia silaha zinazounda uwezo wa kijeshi wa mataifa. Pia ujenzi wa kisasa hauwezekani bila chuma cha pua.

Daraja la reli nchini Argentina ilitengenezwa kwa kutumia feleji.
Mnara wa Eiffel mwenye kimo cha mita 300 ilikuwa jengo kubwa la dunia; imetengenzewa kwa chumapua tu.
Chumapua moto katika hali ya kiowevu yamwagwa kutoka jiko lake.

Chuma cha pua ni ngumu kushinda chuma tupu isiyo na kaboni. Siku hizi kuna pia aloi za chumapua ambamo dutu tofauti na kaboni hutumiwa.

Historia ya chumapua

hariri

Kutengenezwa kwa chumapua kulikuwa sanaa ya pekee kwa karne nyingi. Silaha kama panga za chumapua zilikuwa bora kushinda panga za chuma cha kawaida. Vilevile vifaa kama visu hata majembe vilidumu kama vilitengenezwa kwa chumapua. Wahunzi walipeana mbinu za kutengeneza chumapua kama siri, kwa mfano kati ya wahunzi wa jadi wa Wahaya wa maeneo karibu na Ziwa Viktoria[1].

Tangu mwaka 1610 viwanda katika Uingereza vilianza kutengeneza chumapua kwa vingi ikaboreshwa katika miaka 100 iliyofuata. Mbinu hiyo ilikuwa msingi wa maendeleo ya Uingereza juu ya mataifa mengine mengi katika mapinduzi wa viwandani. Mashine zote zilitengenezwa kwa chumapua.

Mnara wa Eiffel ulikuwa jengo kubwa la kwanza lililoundwa kwa chumapua pekee. Meli za chumapua zilichukua nafasi ya jahazi za awali za ubao.

Tabia za chumapua

hariri

Tabia za chumapua hutegemea na kiasi cha kaboni ndani yake. Kiasi kikubwa cha kaboni husabibisha aloi kuwa ngumu zaidi lakini inavunjika kwa urahisi pia. Kiasi kidogo cha kaboni husababisha chumapua kuwa laini zaidi lakini inanapukia zaidi.

Chumapua cha kawaida huhitaji kinga dhidi ya kutu kama vile rangi au kupakwa kwa zinki.

Nyongeza za kromi zababisha chumapua kutoshika kutu. Hivyo vyombo vya chakula kama vile nyuma, visu au vijiko hutengenezwa na aloi hiyo, pia vifaa vya madaktari kama vile visu vya upasuaji.

Tanbihi

hariri
  1. Peter Schmidt and Donald H. Avery: Complex Iron Smelting and Prehistoric Culture in Tanzania, Science Journal, New Series, Vol. 201, No. 4361 (Sep. 22, 1978), pp. 1085-1089 online hapa

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuma cha pua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.