Tibursi, Valeriani na Masimo

Tibursi, Valeriani na Masimo (walifariki mjini Roma, Italia, 229) walikuwa wanaume walioongokea Ukristo. Kwa sababu hiyo waliteswa na kuuawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo, chini ya kaisari Alexander Severus[1].

Mchoro wa Francesco Botticini: Wat. Sesilia, Valeriani na Tibursi.

Inasemekana Valeriani alikuwa mume wa Sesilia ambaye alimvuta katika Ukristo, naye akamvuta ndugu yake, Tibursi. Walipokamatwa, afisa Masimo aliamua kuwafuata akauawa siku chache baadaye[2].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 14 Aprili[3] au 22 Novemba[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.