Uasi wa Mabondia
Uasi wa Mabondia (kwa Kiingereza: Boxer Rebellion) ulikuwa tukio kubwa la China miaka 1900 na 1901, ambapo kundi la wazalendo lilitumia nguvu ili kufuta athari ya kigeni nchini mwao.
Wageni nchini China
haririWakati huo nchi nyingi za nje zilikuwa zikitawala sehemu za China, zikiwemo hasa Japani, Ufalme wa Muungano, Ujerumani na Russia. China ilikuwa imeshindwa nazo mara nyingi ikawa inadhalilishwa.
Mabondia
haririWalioitwa na Wazungu "Boxers", yaani "Mabondia", walikuwa raia wa China waliochukia hali hiyo na kwa sababu hiyo walitaka kupigania uhuru kamili kwa kufukuza wageni wote na hata baadhi ya Wachina wenzao. Jina lilitokana na sanaa ya mapigano iliyotumiwa na wazalendo. Waliungwa mkono na wananchi wengi wakapigana hadi Beijing. Kati ya waliouawa nao kuna wamisionari 200 na Wakristo wenyeji 32,000.
Siku 55 huko Peking
haririJapani, Russia, Ufalme wa Muungano, Ufaransa, Marekani, Ujerumani, Austria-Hungaria na Italia walikubaliana kuwazuia Mabondia wasiiingie katika sehemu zao za mji huo. Hapo malkia Dowager Cixi alitangaza vita dhidi yao akatuma jeshi la China kusaidia Mabondia.
Walipigana siku 55, lakini hatimaye wakashindwa. Wageni walifanya sherehe, wakazungukazunguka wakiiba mali ya wenyeji na kubaka wanawake. Jemadari wao alikasirika lakini alishindwa kuwazuia.
Matokeo
haririWashindi walidai Wachina pesa na maeneo mengine pamoja na uuaji wa Mabondia wote.
Mwaka 1911 nasaba ya Qing iliangushwa na Jamhuri ya China ilitangazwa, lakini athari ya kigeni iliendelea, hasa kutoka Japani.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uasi wa Mabondia kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |