Ubatizo wa Bwana
Ubatizo wa Bwana ni sikukuu ya liturujia inayoadhimisha fumbo la Yesu kubatizwa na Yohane Mbatizaji katika mto Yordani kabla hajaanza utume wake mwenyewe.
Ndiyo sababu inatimiza kipindi cha Noeli kinachoadhimisha kwa muda mfupi miaka yote ya maisha yaliyofichika ya Yesu, mingi ikiwa aliitumia kama seremala kijijini Nazareti.
Kwa kuwa Yesu aliacha maisha hayo akaanza utume wake miezi tu baada ya Yohane Mbatizaji, jamaa yake, kuwatikisa Wayahudi wote akihubiri wawe tayari kwa ujio wa mtu mkubwa zaidi, akisema, “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto” (Math 3:11).
Viungo vya nje
hariri- media kuhusu Baptism of Jesus Christ pa Wikimedia Commons
- Baptism of Jesus - Catholic Encyclopedia
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ubatizo wa Bwana kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |