Kugeuka sura

(Elekezwa kutoka Yesu Kugeuka Sura)

Yesu kugeuka sura ni sikukuu ya liturujia ya Ukristo inayoadhimisha fumbo la maisha ya Yesu linalosimuliwa katika Agano Jipya[1], hususan katika Injili Ndugu (Math 17:1–9, Mk 9:2-8, Lk 9:28–36) na katika 2 Pet 1:16–18[1].

Mozaiki ya Kugeuka sura, Monasteri ya Mt. Katerina, Mlima Sinai, Misri.
Kugeuka sura katika Injili ya Marko, 1300.
Mchoro wa karne ya 12.
Kugeuka sura kadiri ya Lodovico Carracci, 1594: wanaoonekana pamoja na Yesu ni Eliya, Musa na Mitume wa Yesu watatu.
Mchoro wa Alexandr Ivanov, 1824.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Kanisa la Kugeuka Sura juu ya Mlima Tabor, Israel, unaohesabiwa na wengi kuwa mahali pa tukio.

Humo tunasoma kwamba Yesu Kristo aliongozana na wanafunzi wake watatu, Mtume Petro, Yakobo Mkubwa na mdogo wake Mtume Yohane, hadi mlima kwa lengo la kusali faraghani.

Huko usiku alianza kung'aa akatokewa na Musa na Eliya waliozungumza naye kuhusu kufariki kwake Yerusalemu.

Kubwa zaidi, Mungu Baba alimshuhudia kuwa Mwana wake mpenzi akawahimiza wanafunzi hao kumsikiliza.[1]

Tukio linaheshimiwa hasa na Ukristo wa Mashariki na wamonaki wanaoliona mwaliko wa kutazama utukufu wa Mungu uliofichama katika malimwengu, kumbe kwa sala unadhihirika kwa macho ya imani.

Fumbo hilo linaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu tarehe 6 Agosti[2]. Pia linazingatiwa katika Rozari kama tendo la nne la mwanga.

Picha hariri

Ukristo wa Mashariki hariri

Ukristo wa Magharibi hariri

Makanisa na monasteri hariri

Tanbihi hariri

  1. 1.0 1.1 1.2 Transfiguration by Dorothy A. Lee 2005 ISBN 978-0-8264-7595-4 pages 21-30
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kugeuka sura kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.