Open main menu

Katika UkristoEdit

Msingi wa tumaini hilo katika Ukristo ni ahadi alizotoa mwenyewe na ambazo zinasomwa katika Injili (Math 24:27; 25:31; Lk 17:30; Yoh 6:39-40).

Ufafanuzi zaidi ulitolewa na Mtume Paulo (Mdo 10:42; 17:31; Rom 2:5-16; 14:10; 1Kor 4:5; 15:23; 2Kor 5:10; Fil 1:6; 1Tim 6:14; 2 Tim 4:1,8; Tito 2:13; 1Thes 5:2; 2Thes 1:5; 2:1-9) na wengineo katika vitabu vingine vya Agano Jipya (1Pet 4:13; Yak 5:7) na baadaye.

Katika Agano Jipya neno ἐπιφάνεια, epiphaneia, kutokea, limetumika mara 5 kuhusiana na kurudi kwa Kristo,[1] kumbe neno παρουσία, parousia, kufika au kuwepo, mara 17.[2][3]

Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli (karne ya 4) ilikiri kwamba "atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu, na ufalme wake hautakuwa na mwisho".

Hata hivyo Wakristo wanatofautiana kuhusu jambo hilo kadiri ya madhehebu yao, lakini pia kadiri ya rai binafsi kuhusu maana halisi ya maneno yake.

Kama Yesu mwenyewe alivyotabiri, jambo hilo litaleta udanganyifu mwingi ambao alitaka wafuasi wake wajihadari usiwapate.

Kweli karne hata karne walitokea watu kutabiri mwaka au hata tarehe ya tukio hilo; tena wengine walisema limeshafanyika, kumbe bado.

Yesu alisema, "Hakuna anayejua siku wala saa". Lakini watu hao walijaribu kutumia namba za Biblia ili kuhesabu itakuwa lini.

Katika UislamuEdit

Katika Islam, عيسى (ʿĪsā, Isa) anaheshimiwa kama mtume na Masihi aliyetumwa kwa Waisraeli (banī isrā'īl) akiwaletea kitabu kipya, Injili.[4]

Quran inazungumzia ujio wa pili wa huyo Yesu katika sura Az-zukhruf (43:61) kama ishara ya siku ya hukumu.[5][6]

Pia kuna Hadithi za Mtume Muhammad zinazotabiri wazi ujio wake.[7][8]

TanbihiEdit

  1. NT usage
  2. Strong's G3952. Blueletterbible.org. Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
  3. CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: General Judgment (Last Judgment). Newadvent.org (1910-10-01). Iliwekwa mnamo 2009-11-21.
  4. The Oxford Dictionary of Islam, p.158
  5. Surah Az-zukhruf.
  6. Tafsir al-Qur'an al-Azim.
  7. "Isa", Encyclopedia of Islam
  8. Sonn (2004) p. 209

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ujio wa pili kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.