Ndugu wa Yesu
Ndugu wa Yesu ni watu wa Israeli wa karne ya 1 wanaotajwa na Agano Jipya, mara nyingi kama wapinzani wa Yesu. Hata hivyo baadaye baadhi yao walishika nafasi muhimu katika Kanisa.
Kati yao wanaotajwa kwa jina ni Yakobo, Yose, Yuda na Simoni (Math 13:55 [1]).
Tangu kale neno "ndugu" limesababisha maswali juu ya uhusiano kati yao na Yesu.
- Wengine wametafsiri neno hilo kadiri ya maana ya Kigiriki cha Kale, yaani ndugu wanaochanga wazazi, walau mmoja[2].
- Wengine wametafsiri neno kwa maana yake asili katika lugha ya Kiaramu, iliyokuwa lugha mama ya Yesu na ndugu zake, ambamo neno lina maana pana kama katika Kiswahili[3] . Pia kwa sababu Kigiriki cha wakati wa Yesu kilitumia mara nyingi neno hilo namna hiyo[4][5].
Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Walutheri wanashika msimamo wa pili pia kwa sababu wanasadiki Ubikira wa kudumu wa Mama wa Yesu, wakimuita Bikira daima.
Tanbihi
hariri- ↑ Greek New Testament, Sacred texts, Matthew 13:55: "οὐχ οὖτός ἐστιν ὁ τοῦ τέκτονος υἱός; οὐχ ἡ μήτηρ αὐτοῦ λέγεται μαριὰμ καὶ οἱ ἀδελφοὶ αὐτοῦ ἰάκωβος καὶ ἰωσὴφ καὶ σίμων καὶ ἰούδας;"
- ↑ Segal, Charles (1999), Tragedy and civilization: an interpretation of Sophocles, uk. 184,
word for 'brother,' adelphos, from a- ('same,' equivalent to homo-) and delphys ('womb,' equivalent to splanchna).
- ↑ Giuseppe Ricciotti, Vita di Gesu Cristo, 3rd ed., Arnoldo Mondadori Editore, Milan, 1962: ‘in Hebraic language there is no specific word for our "cousin". Also, in Hebraic Bible the words "brother" and "sister" are frequently used referring to people with very different degree of kinship.’
- ↑ The International Standard Bible Encyclopedia p281 ed. Geoffrey W. Bromiley
- ↑ Strong's Greek: 80. ἀδελφός (adelphos) -- a brother. Iliwekwa mnamo 16 Julai 2020.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
hariri- Bethel, Florentine (1907) [Robert Appleton Company], "The Brethren of the Lord", The Catholic Encyclopedia, juz. la 2, New York: New advent
- Funk, Robert W (1998), The acts of Jesus: the search for the authentic deeds of Jesus, The Jesus Seminar, San Francisco: Harper, ISBN 978-0-06062978-6
Marejeo mengine
hariri- Kilgallen, John J (1989), A Brief Commentary on the Gospel of Mark, Paulist.
- Tabor, James D (2006), The Jesus Dynasty, Simon & Schuster.
- Aslan, Reza (2014), Zealot: The Life and Times of Jesus of Nazareth, HarperCollins Publishers India, ISBN 978-9351360773
Viungo vya nje
hariri- Jerome (c. 383), "The Perpetual Virginity of Blessed Mary – Against Helvidius", katika Philip Schaff; Henry Wace; Kevin Knight (whr.), Nicene and Post-Nicene Fathers, Second Series, Vol. 6, Translated by W.H. Fremantle, G. Lewis and W.G. Martley, Buffalo, New York: Christian Literature Publishing Co. (retrieved from New Advent)
- Hunter, David G. (Spring 1993). "Helvidius, Jovinian, and the Virginity of Mary in Late Fourth-Century Rome". Journal of Early Christian Studies. 1 (1): 47–71. doi:10.1353/earl.0.0147. S2CID 170719507. Iliwekwa mnamo 2016-08-30.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - John J Rousseau, Rami Arav (1995), "Jesus' Family Tree", Jesus and His World, Augsberg Fortress (retrieved from PBS)
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ndugu wa Yesu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |