Ukoo wa Yesu
Ukoo wa Yesu unapatikana katika vitabu viwili vya Agano Jipya: Injili ya Mathayo ambayo inaorodhesha vizazi kuanzia Abrahamu hadi kwa Yosefu (mume wa Maria), na Injili ya Luka inayorudi nyuma kuanzia Yosefu hadi kwa Adamu, aliyeumbwa na Mungu mwenyewe.
Injili hizo zote mbili zinasisitiza kwamba Yosefu si mzazi wa Yesu, kwa kuwa Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Pia zinasisitiza kwamba Yesu ni Mwana wa Daudi, yaani kwa njia ya Yosefu, ambaye kinasaba anatokana na mfalme huyo maarufu wa Agano la Kale, ana haki ya kurithi cheo chake.
Hata hivyo majina mengi ni tofauti katika orodha hizo mbili, kiasi kwamba wataalamu wanatoa maelezo mbalimbali kuhusiana na desturi za Israeli wakati ule, kwa mfano katika kutumia orodha ya vizazi, na kutokana na malengo ya Wainjili hao[1][2], ambao wote wawili walitaka kusisitiza kihisabati kwamba Yesu amefika kwa wakati mwafaka uliopangwa na Mungu kwa makini (vizazi 14x3 kadiri ya Mathayo; 7x11 kadiri ya Luka).
Akiwaandikia Wayahudi, mwinjili Mathayo alitaka kusisitiza kwamba Yesu ni Daudi mpya, lakini pia mrithi wa Abrahamu katika kuwa baraka kwa mataifa yote.
Akiwaandikia watu wa mataifa, mwinjili Luka alitaka kuonyesha kwamba Yesu ni mwana wa Adamu, hivyo anahusiana na binadamu wote.
Tanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Information on the Michelangelo frescoes
- Multiple translations
- Anne Catherine Emmerich, Life of the Blessed Virgin Mary
- Bible Study Manual on Genealogy of Jesus
- Genealogy of Jesus at Complete-Bible-Genealogy.com
- Dueling Genealogies Why there are two different genealogies for Jesus.
- New Light on the Genealogies of Jesus
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ukoo wa Yesu kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |